Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Serikali imesema itaendelea na jitihada za kuhakikisha inajenga vituo vingi vya afya na kuboresha miundombinu ikiwemo vifaa tiba na usafiri ili kusaidia kila mtu anapohitaji huduma kat za afya anahudumiwa vizuri na watoa huduma.

Ameyasema hayo leo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo Mai 17, 2024 katika hafla ya ugawaji bajaji 18 na vibao vya kupima Urefu watoto walio chini ya umri wa miaka mitano vifaa hivuo ni kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa huduma na kutekeleza afua za lishe.

Vipimo hivi vitakwenda kusaidia kujua mtoto kuanzia anapozaliwa je yuko na uzito unaostahili ili aweze kusaidiwa kwenye eneo hilo hivyo fedha zilizotengwa ni zaidi ya shilingi milioni 300 ambazo zinaenda kwenye afua za lishe na miongoni mwa fedha hizo milioni 22 zimekwenda kununua vipimo hivi kwa ajili ya watoto” amesema Mkuu wa Wilaya

Mpogolo amesema kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM imeahidi kuboresha huduma za Afya na moja ya maboresho ni eneo la ujenzi wa miundombinu ambapo Mhe Rais Dkt Samia ametenga zaidi ya Dolla bilioni 26 kuboresha miundombinu katika halmashauri ya jiji la Ilala na ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vikubwa viwili vya afya cha Mchikichini kinachogharimu kiasi cha fedha bilion 5 na kituo cha Mzinga mradi wenye thamani ya bilioni 2.5 na na hadi sasa kuna vituo vya afya zaidi ya 10 na vipo katika hatua za mwisho kukamilika .

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Ilala Dkt Zaituni Hamza amesema moja ya shughuli zao ni kutekeleza vipaumbele muhimu vya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kuhakikisha huduma za afya zinatolewa vizuri.

“Tulitengewa fedha na katika fedha hizo hivyo tumenunua bajaji 18, ztakazo
tumika na watumishi ikiwemo 3kufutilia makuzi ya mtoto nyumba kwa nyumba ,3 chanjo,3 shughuli za kutokomeza Malaria Nchini ,3ustawi wa jamii ‘”amebainisha Dkt Zaituni

Aidha watumishi wote waliokabidhiwa vifaa hivyo wameombwa kuvitunza vizuri na kuvitumia kwa mlengo uliokusudiwa.