Habari za Kitaifa

Abambikiziwa uanachama mfuko wa jamii

Uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa miaka minne umeshindwa kulipa mafao ya kustaafu ya askari polisi aliyelitumikia jeshi hilo kwa miaka 33, kisa kabambikizwa uanachama katika mfuko mwingine. Thomas Njama, amestaafu Jeshi la Polisi mwaka 2015 akiwa Kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu mkoani Arusha. Amesema PSPF wanatakiwa kumlipa kiinua mgongo cha Sh 47,162,022 na ...

Read More »

Mwalimu mtuhumiwa mauaji ni Mkenya

Shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo Himo, Moshi mkoani Kilimanjaro inatuhumiwa kuajiri mwalimu raia wa Kenya asiyekuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Mwalimu Laban Nabiswa, ni mshtakiwa wa tatu katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi Humphrey Makundi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika Shule hiyo ya Scolastica. Laban amekiri mahakamani kuishi na kufanya kazi nchini isivyo halali ...

Read More »

Rushwa ya ngono yamtumbukia mwalimu

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jabarhila, iliyopo Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, Mwatanda Omari (37), amehukumiwa kwenda jela miezi 12 kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono. Mwalimu Omari alitenda kosa hilo Machi 9, 2017 kwa kumuomba rushwa hiyo mzazi wa mwanafunzi katika shule hiyo. Jina la mzazi limehifadhiwa. Mzazi alikuwa anaomba uhamisho wa mtoto kutoka shuleni hapo kwenda Dar es ...

Read More »

Wamdanganya Magufuli

Kashfa imegubika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi mwaka huu yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya. Kashfa hiyo imekikumba Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU). Ndani ya chama hicho, baadhi ya viongozi wake wanadaiwa kuwasilisha jina la kigogo asiyestahili kuwa mfanyakazi bora, akapewa mkono na Rais Dk. John Magufuli na kukabidhiwa cheti cha mfanyakazi bora na zawadi ya ...

Read More »

Fedha za wastaafu zakwapuliwa

Shilingi bilioni 1.2 zikiwa ni fedha za malipo ya mafao ya walimu wastaafu katika Mkoa wa Mara zinadaiwa kukwapuliwa na mafisadi, Gazeti la JAMHURI linaripoti. Mamilioni hayo ya fedha yameelezwa kuchukuliwa kupitia njia ovu ya mikopo hewa. Baadhi ya viongozi wa serikali wanaosimamia masilahi ya watumishi wanahusishwa na tuhuma hizi. Wanadaiwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara kufanikisha mchezo huo. Waathirika ...

Read More »

Dengue mtihani

Si kila homa ni malaria! Kauli hii inapaswa kuzingatiwa hasa kipindi hiki ambacho ugonjwa wa homa ya dengue unatajwa kushika kasi jijini Dar es Salaam. Serikali imethibitisha ugonjwa huo kusambaa kwa haraka katika wilaya za Ilala, Kinondoni na Ubungo. Kutokana na hali hiyo, wakazi wa maeneo hayo wametakiwa kuwahi katika vituo vya afya ama hospitalini wanapohisi mabadiliko katika miili yao ...

Read More »

Mazito ya Mengi

Mfanyabiashara maarufu nchini na kimataifa, Reginald Mengi, amekuwa na maisha yenye mengi, kuanzia mwenendo wake binafsi na mwenendo wake ndani ya jamii alimoishi. Undani wa maisha yake umejibainisha katika kitabu chake cha hivi karibuni kinachoitwa “I Can, I Must, I Will” chenye kaulimbiu ya “The spirit of success”. Mengi, katika kitabu hicho amepata kukizungumzia kifo, hasa baada ya kufariki dunia ...

Read More »

Avamia ardhi ya mwenzake kibabe

Kumeibuka mgogoro wa ardhi katika Kisiwa cha Juma Kisiwani, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, unahusu ekari 26 zinazomilikiwa na mfanyabiashara wa madini, Baraka Chilu; lakini mfanyabiashara wa samaki, Joseph Njiwapori, anadaiwa kulivamia eneo hilo. Serikali ya Kijiji cha Juma Kisiwani imelifikisha suala hilo Polisi Wilaya ya Sengerema. Mwenyekiti wa Kijiji cha Juma Kisiwani, Tibahikana Maharage, ameliambia Gazeti la JAMHURI kuwa Njiwapori ameingia isivyo ...

Read More »

CCM: CAG safi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema ukaguzi na udhibiti wa ndani ya chama hicho kwa sasa ni zaidi ya kile kilichobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Kwa mujibu wa Dk. Bashiru, Kamati ya Kuhakiki Mali za CCM aliyoiongoza kwa takriban miezi mitatu ilibaini mengi zaidi ...

Read More »

CAG apigilia msumari Tarime

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, imesadifu kile kilichoandikwa na Gazeti la JAMHURI katika toleo namba 385 kuhusu ubadhirifu wa fedha za maendeleo katika Wilaya ya Tarime. JAMHURI katika toleo hilo liliandika kuhusu mgogoro wa kiuongozi na tuhuma za upotevu wa fedha za maendeleo zikimhusu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Glorious Luoga. ...

Read More »

Mikoa 3 dhaifu utoaji chanjo

Mikoa ya Katavi, Shinyanga na Tabora inaongoza nchini kwa kuwa nyuma katika kuwapatia chanjo watoto wenye umri chini ya miaka miwili. Akizungumzia hali hiyo hivi karibuni mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Health Promotion Tanzania, Peter Bujari, amesema Mkoa wa Katavi umekuwa na kiwango cha asilimia 54.1 kwa watoto waliopata ...

Read More »

CUF njia panda

Wabunge 24 wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye amehamia Chama cha ACT – Wazalendo, wataendelea kushikilia ubunge wao hali inayoiweka CUF njia panda, JAMHURI limeelezwa. Wabunge hao walijikuta katika mtihani wa kuchagua ama kuachana na ubunge wao wamfuate Maalim Seif ACT au wabaki CUF kulinda ubunge wao hadi ...

Read More »

Ujenzi Ziwa Victoria wazua jambo

Mradi mkubwa wa maji unaojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) umeingia lawamani baada ya kampuni inayojenga kuanza kumwaga vifusi vya udongo ndani ya Ziwa Victoria. Hali hiyo inayodaiwa kusababisha uchafuzi wa mazingira, inalenga kujenga barabara ya udongo ziwani ambayo itarahisisha ufungwaji wa mitambo ya kusambaza maji ya kunywa kwa wananchi. Taarifa zinabainisha hadi sasa zaidi ya ...

Read More »

Ngorongoro inavyotafunwa

Wakati Rais Dk. John Magufuli akihimiza kubana matumizi ya idara na taasisi za serikali, hali ni tofauti kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Shilingi bilioni 1.1 zimetumika kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 kuhudumia vikao vya bodi hiyo. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, bodi imekaa vikao 20 tofauti na utaratibu unaoagiza vikao viwe vinne kwa ...

Read More »

Aibu Mkwakwani

Mpita Njia (MN) anatanguliza salamu zake za Sikukuu ya Pasaka kwa Wakristo wote nchini ambao bila shaka wataungana na wenzao wa maeneo mengine duniani kwa ajili ya siku hiyo ya kiimani kwao. Tukiachana na hayo, kama ilivyo kawaida yake, MN wiki hii alikuwa mkoani Tanga kwa ajili ya shughuli zake za ujenzi wa taifa. Loh! Tanga kuna mengi yaliyo mazuri, ...

Read More »

Jiji waomba fursa mabasi 100 ‘mwendokasi’

Uongozi wa Jiji la Dar es Salaam umeiomba Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwapa kibali cha kuongeza mabasi ya usafiri wa haraka (mwendokasi) katika Jiji la Dar es Salaam. Lengo la kuomba kibali hicho ni kutaka kushirikiana na mkandarasi aliyepewa dhamana ya kuendesha mradi huo ili kuboresha huduma ya usafiri ya ...

Read More »

Nondo feki zazua balaa Siha

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) imeanza uchunguzi kuhusu tuhuma zinazoikabili kampuni moja ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi mkoani Kilimanjaro, inayodaiwa kuiuzia serikali nondo feki zisizo na ubora. Kampuni hiyo ambayo kwa sasa jina lake tunalihifadhi baada ya mkurugenzi wake kutopatikana, ilishinda zabuni ya kuuza nondo kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha ...

Read More »

‘Tunateseka’

Mahabusu wawili wamemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, wakidai wanashtakiwa kwa kosa la kuua ilhali aliyefanya mauaji hayo na kukiri yuko huru uraiani. Michael Laizer na Lucas Mmasi, wanashikiliwa katika Gereza Kuu Mkoa wa Arusha, Kisongo, tangu mwaka 2015 wakikabiliwa na shtaka hilo wanalodai kuwa ni la kubambikiwa. Barua hiyo ambayo JAMHURI imeona nakala yake, ...

Read More »

‘Mjadala wa CAG, Bunge si utekelezaji wa ilani’

Mpita Njia, maarufu kwa ufupisho wa MN, kwa wiki nzima iliyopita amesikia mijadala mingi katika mitaa kadhaa aliyopita wakati wa shughuli zake za kawaida za kila siku. Mijadala hii ilihusu Azimio la Bunge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Bunge limeazimia kutokufanya kazi na msomi ...

Read More »

Rais Magufuli azima umegaji hifadhi

Rais John Magufuli amekataa mapendekezo ya wanavijiji katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, ya kutaka wamegewe ardhi katika Pori la Akiba la Selous. Amewaonya wanasiasa ambao hutumia ghiliba wakati wa kampeni kwa kuahidi kuwa wakichaguliwa watahakikisha wanamega maeneo ya hifadhi na kuwapa wananchi. Rais Magufuli yumo katika ziara ya siku tano mkoani Ruvuma. Amesema Tanzania ina ardhi kubwa ambayo ikitumiwa ...

Read More »

BoT wamtosa mteja aliyeibiwa Ecobank

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema haiwezi kufanya chochote kumsaidia mfanyabiashara aliyeibiwa fedha kwenye akaunti yake katika Ecobank, Tawi la Uhuru, jijini Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) imeitia hatiani Ecobank Tanzania Limited kwa kumwibia mteja wake, Kampuni ya Future Trading Limited, Sh milioni 66 kutoka kwenye akaunti yake. Fedha hizo zimeibwa kwenye akaunti hiyo kupitia ...

Read More »

Tuhuma za ufisadi zatanda Kwimba

Kumeibuliwa tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza. Miradi mitano ya ujenzi imekwama. Miradi iliyokwama ni ujenzi wa vyumba vya maabara wa mwaka 2014; kliniki ya mifugo na bwalo la chakula, iliyoanza mwaka 2016. Mingine ni ujenzi wa nyumba tatu za walimu katika shule za msingi za Itegamatu, Ilula na ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons