Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu wakati wa hafla ya Chakula cha jioni, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka nchi mbalimbali wakielekea kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.
Wakuu wa nchi mbalimbali pamoja na Viongozi wengine wakiwa kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi hao wanaoshiriki Mkutano wa Rasilimali watu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi pamoja na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova kabla ya hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.