Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amempokea Rais wa Hungary, Katalin Novak katika Ikulu ya Magogoni,Dar es Salaam leo Julai 18, 2023.

Rais huyo amewasili jana usiku Julai 17, 2023 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Stegoma Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jullius Nyerere (JNICC).

Katika ziara yake ya siku tatu nchini rais huyo amefika Ikulu ya Dar es Salaam na kupokelewa na rais Samia ambapo baadaye wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari.
Kama ilivyo kwa Rais Samia Katalin Novak ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais wa Hungary ambapo aliingia madarakani mnamo Mei 22, 2023.
Aidha ni Rais wa kwanza kutoka taifa hilo kufanya ziara nchini Tanzania ambapo ziara hiyo itakamilika Julai 20,2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Hungary Mhe. Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Hungary Mhe. Katalin Novák wakati wakiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na mgeni wake Rais wa Hungary Mhe. Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Hungary Mhe. Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.