Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwekeza katika utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi kupitia vipindi vya ubunifu, akisema hatua hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali za kujenga uchumi jumuishi na kuongeza uelewa wa kifedha kwa Watanzania.
Ameyasema hayo leo Julai 22,2026 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa CRDB Zongo Mchongo msimu wa nne ambapo Amesema
kuwa elimu ya fedha ni msingi muhimu wa kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi kuhusu uwekezaji, biashara, matumizi na utunzaji wa fedha.
” CRDB ni Benki iliyofanikiwa Sanaa ikiwa kufikisha elimu hiyo kwa njia rahisi kupitia televisheni, mitandao ya kijamii na ushirikishwaji wa wasanii, wanamichezo na watengeneza maudhui fursa za kiuchumi “Amesema Waziri .
Makonda amesema NI vyema Benki hiyo kuwatumia watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii kusambaza elimu ya fedha kwa wananchi wengi kuelewa fursa za kiuchumi, huku yakichochea ajira na kuongeza kipato kwa vijana wanaotumia vipaji vyao kutengeneza maudhui.
Aidha, amewataka Watanzania kuacha kufuatilia taarifa zisizo na manufaa na badala yake kutumia muda kujifunza masuala ya fedha, biashara na uwekezaji ili waweze kunufaika na fursa zinazozalishwa na Serikali pamoja na taasisi za kifedha.
Akizungumzia matukio makubwa yanayotarajiwa kufanyika nchini, Afconi,na Mashindano ya Urembo(Miss World )Makonda alisema wananchi wanapaswa kujiandaa kuyatumia kama fursa za kuongeza kipato, akisisitiza kuwa mafanikio hayo yatawezekana endapo elimu ya fedha itaendelea kuwafikia watu wengi zaidi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt Abdulmajid Nsekala Amesema benki hiyo imebadili mkakati wake kutoka kuuza huduma za kifedha pekee na sasa inaweka nguvu kubwa katika kujenga jamii yenye maarifa ya fedha ili iweze kufanya maamuzi sahihi katika matumizi ya huduma za kifedha.
Nsekela amesema kipindi cha Zogo Mchongo ni sehemu ya mkakati huo, ambapo kupitia msimu wa nne wananchi watapata elimu kuhusu Mikopo,uhifadhi fedha,kufanya miamala kidigitali






