Mwenyekiti wa CHADEMA meshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kushoto), akisisitiza jambo mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, wakati wa kikao cha Msajili na viongozi waandamizi wa CHADEMA leo jijini Dar es Salaam. Kikao cha Msajili na CHADEMA ni juhudi za ofisi hiyo kuimarisha hali ya kisiasa hususan demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini. (Picha na ORPP)
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati) na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (kulia) wakimsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kwanza kushoto) wakati wa kikao cha Msajili na chama cha CHADEMA chenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na ORPP)
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kulia) akiteta jambo na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati), baada ya kumaliza kikao chenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu wa CHADEMA ndugu John Myika. (Picha na ORPP)

By Jamhuri