Makala

Tangu lini wapinzani wanawapenda wananchi?

Vyama vya upinzani vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika Bunge Maalum la Katiba vimesusia vikao vya bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu.

Wapinzani wametoa sababu zao za kuchukua hatua hiyo. Kwa mfano, wamesema Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, wametoa vitisho kwamba kukiwapo Serikali tatu Jeshi litachukua nchi.

Read More »

Nani analinda bodaboda Dar?

Moja ya mambo yaliyomfurahisha Mkata Mitaa (MM) ni hatua iliyochukuliwa na Serikali kupiga marufuku pikipiki maarufu kwa jina la ‘bodaboda’, mikokoteni (makuta), baiskeli na bajaj kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam.

MM amefurahishwa na mpango huo kutokana na boda boda kuwa kero kwa waendesha magari na waenda kwa mguu wanaotumia barabara za katikati ya jiji.

Read More »

Vituko vya DC Geita vyaongezeka – 3

DC adaiwa kumtisha Roboyanke

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnyara, Makoye Roboyanke (CCM), ambaye inadaiwa alivuliwa madaraka hayo na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie, amedai kuwa Septemba 10, 2013 mchana akiwa shambani kwake kijijini hapo, alipokea simu ya vitisho kutoka kwa kiongozi huyo wa Serikali.

“Alijitambulisha kwa jina moja la Mangochie na kwamba ndiye Mkuu wa Wilaya ya Geita, akaniuliza jina langu nami nikamjibu… akaniuliza ninachofanya kwa wakati huo na kazi yangu hasa ni nini, nikamwomba arekebishe kauli, na baada ya kurekebisha kauli na kuniuliza maswali ya msingi nilimpa ushirikiano.

Read More »

KAGAME NI MTIHANI

Viongozi Maziwa Makuu waufanye kwa Uangalifu - 4

 

Tangu Kagame na RPF waitwae Rwanda ni wazi kuwa nchi hiyo inapokea fadhila za Washington DC kuliko nchi yoyote nyingine katika Maziwa Makuu.

Misaada ambayo inatoka Marekani na Uingereza kuelekezwa Kigali ni mingi na ya aina mbalimbali. Kwa hesabu rahisi misaada hiyo inafafanua ustawi wa uchumi wa Rwanda tunaouona leo.

Read More »

JWTZ: Tunavifyeka vikundi vya waasi Congo

Baada ya ushindi dhidi ya Waasi wa March 23 (M23), Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na Majeshi ya Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) limesema hakuna kikwazo chochote cha  kuwaondoa waasi wa ADF- NALU  na FDRL.

Read More »

Ilikosewa kuruhusu UKAWA bungeni

Wiki iliyopita wanachama wa unaotajwa kuwa ni Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) walisusia kushiriki vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.

UKAWA hiyo inaundwa na wanachama wa vyama vya upinzani miongoni mwa wajumbe wanaounda bunge hilo lililokabidhiwa jukumu nyeti la kuwezesha upatikanaji wa Katiba bora ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Read More »

Mkurugenzi Bandari anahujumu Bodi

Uchunguzi uliofanywa na gazeti JAMHURI umebaini taarifa nyingi za uonevu katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Uonevu na ubabe wa Mkurugenzi, Madeni Kipande, haukuishia kwa wafanyakazi pekee, bali anaburuza hadi wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Hali hii inahujumu uchumi wa nchi. Baada ya kuona hatari inayolinyemelea Taifa, mmoja wa wakurugenzi aliamua kuwasilisha hoja ya kumuondoa Kipande madarakani, lakini kwa bahati mbaya kutokana na mizizi mizito aliyonayo Kipande, wenzake watano ndiyo walioondolewa kwenye Bodi, kwa Waziri Dk. Harrison Mwakyembe kuvunja Bodi hiyo na kuteua wateule awapendao. Ifuatayo ni taarifa husika katika tafsiri isiyo rasmi. Endelea….

Read More »

Nyalandu aanza kuliliza Taifa

*Marekani yapiga marufuku nyara kutoka Tanzania Uamuzi tata na wa kijazba wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, umeanza kuleta athari kwa tasnia ya uwindaji wa kitalii nchini. Marekani imepiga marufuku nyara zinazotokana na ndovu kutoka Tanzania kuingizwa nchini humo. Hilo ni pigo kubwa kwa uchumi wa Tanzania. Kwa mujibu wa Shirika la Samaki na Wanyamapori la Marekani (US ...

Read More »

Uchaguzi Chalinze ni huru, lakini si wa haki

Hivi karibuni nilishiriki mjadala unaohusu uamuzi wa Ridhiwani Kikwete kugombea ubunge Jimbo la Chalinze.

Kama ilivyo ada, mijadala ya aina hii mara zote imekuwa na mvuto. Kumekuwapo hoja kwamba wanaohoji uhalali wa mtoto wa Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge kupitia chama kinachoongozwa na babaake, ni wivu na husda!

Lakini wapo wanaoona kuwa kitendo hicho, ingawa ni haki yake ya kikatiba kama walivyo Watanzania wengine, hakiwezi kutolewa maelezo hata kikaweza kueleweka kwa wananchi walio wengi.

Sikukusudia kuendelea na mjadala huu kwa sababu tayari nilishaweka bayana faida na hasara za uamuzi wa Ridhiwani. Hata hivyo, makala kadhaa zilizoandikwa kwenye magazeti zimenifanya nirejee kutetea hoja yangu.

Read More »

KAGAME NI MTIHANI

Viongozi Maziwa Makuu waufanye kwa uangalifu   Je, ulipata kujua undani wa kisaikolojia na mazingira-mali vilivyosababisha dunia kuingia kwenye Vita Kuu ya Pili miaka ya 1939-1945? Kama unajua karibu tutafakari. Kama hujui naomba nikueleze kwa kifupi. “Sera ya huruma iliyofanywa na nchi za Marekani, Uingereza na Ufaransa kumbeba Mzungu mwenzao, Ujerumani, zilitengeneza uendawazimu wa kifashisti chini ya jinamizi ‘unazi’. Baadhi ...

Read More »

MKATA MITAA

WAWATA St. Joseph na bei za vyakula za ‘kitalii’

Kwa kawaida watu wanyonge wamezitambua nyumba za ibada kama sehemu ya ukombozi! Haishangazi kuwaona kina mama, kina baba, watoto, wazee na watu wasiojiweza wakikimbilia makanisani na misikitini kunapotokea vurugu.

Read More »

FASIHI FASAHA

Mandela  ataenziwa au atakumbukwa?

Ni muda wa wiki tatu sasa, dunia imepata mzizimo na simanzi kutokana na kifo cha mtoto wa Afrika, shujaa, mpenda haki na usawa na kipenzi cha dunia, mtoto huyo ni Nelson Mandela. “Madiba.”

Read More »

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

 

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (11)

 

Katika sehemu ya kumi, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema kwa hiyo Waziri Mkuu alipomwambia Rais kwamba hoja ya Serikali Tatu ikijadiliwa Bungeni yeye mwenyewe atakuwa na utatizi wa uamuzi, alikuwa anajisemea kweli yake. Alikuwa katika hali hii ya “dilemma”. Baadaye, kama tunavyojua, alipoambiwa kuwa asipokubaliana na wenzake ataachwa katika mataa, aliamua kusarenda na wote wakaunga mkono hoja ya Utanganyika.

Ifuatayo ni sehemu ya kitabu cha Mwalimu Nyerere alichokiandika mwaka 1994 cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Endelea...

 

Hawa si watu wajinga, na wala  si wapumbavu; wanajua wafanyalo. Wamefanya uamuzi huu wakijua matokeo yake. Kwa hawa sasa, makosa ya “Wazanzibari” yawe ya kuvunja Katiba au ya aina nyingine, kwao sasa ni faraja; ni hoja ya kudai Utanganyika. Hawa hawawezi tena kutaka makosa hayo yazungumzwe na yasahihishwe; maana yakisahihishwa kama lilivyosahihishwa lile la OIC msingi wake wa hoja yao utabomoka.

Read More »

Viongozi waige uzalendo wa Rais Jakaya Kikwete

 

Tumeambiwa kwamba Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limesitisha mashindano ya Miss Utalii baada ya kuona uendeshaji wa mashindano hayo umekosa uzalendo na hauzingatii utamaduni wa Tanzania.

Read More »

JAMHURI YA WAUNGWANA

Ujasiri huu wa ‘Wasukuma’ utufumbue macho Watanzania

Diwani wa Kisesa, Clement Mabina, ameuawa. Waliomuua ni wananchi, pengine wakiwamo wapigakura wake. Tumeziona picha zikimwonesha Mabina akiwa amepasuliwa kichwa na mwili wake ukiwa ndani ya dimbwi la damu na kando yake kukiwa na mawe makubwa. Waliomuua walifanya hivyo kana kwamba wanamuua mnyama hatari aliyeingia kwenye himaya ya binadamu! Ni jambo la kusikitisha.

Read More »

FIKRA YA HEKIMA

 

Wabunge hawa hawatufai

 

Nianze kwa kuwapa pole mawaziri Shamshi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Dk. Mathayo David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), waliopitiwa na rungu la Rais Jakaya Kikwete la kuvuliwa nyadhifa hizo, wiki iliyopita. Huo ndiyo uwajibikaji wa kisiasa.

Read More »

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (9)

Katika sehemu ya nane, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema Rais ndiye aliyekiri kosa la Zanzibar kuingia katika OIC na pili ndiye aliyelazimika kukiri kule Dodoma kwamba utaratibu wa kushughulikia hoja ya Utanganyika ulikosewa lakini mawaziri wake mara zote mbili walitulia tu nakumuacha Rais ndiye akiri kosa na kubeba lawama. Ifuatayo ni sehemu ya kitabu cha Mwalimu Nyerere alichokiandika mwaka 1994 cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Endelea...

 

Katiba ya nchi yetu, na utaratibu tunaojaribu kujenga, vinataka kuwa katika hali kama hiyo, Mawaziri ndiyo wawajibike, na hivyo kumlinda Rais, si Rais awajibike, na kuwalinda Mawaziri wake, na tena  kwa kosa ambalo si lake. Watu walioshindwa uongozi Bungeni, hata tukafikishwa hapa tulipo leo, ni Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa CCM.

Read More »

FASIHI FASAHA

Lissu ni malaika, waziri au mwanasiasa?


Ni takriban wiki tatu sasa tangu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kipate mtikisiko mkubwa, mithili ya pata shika na nguo kuchanika, baada ya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kuwavua nyadhifa zote viongozi wake watatu.

Read More »

KONA YA AFYA

Sababu za kupungua nguvu za kiume -5


Wiki iliyopita, Dk. Khamisi Ibrahim Zephania alizungumzia kwa kina homoni ya kiume na umuhimu wake katika tendo la ndoa. Sasa endelea kumfuatilia zaidi…

Panahitajika ubongo, neva, homoni, mishipa ya damu, tezi [glands], utendaji mzuri wa figo, ini, baadhi ya misuli na viungo chungu nzima ndani ya mwili kama tutakavyoona katika makala zetu za mbele.

Read More »

Milima, mabonde ya Nelson Mandela

 

Mpigania haki za weusi na alama kuu ya udhalimu wa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Mzee Nelson Madiba Mandela, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu, kutokana na maambukizo ya mapafu kushindwa kutengamaa.

Read More »

Nyerere na Uhuru wa Tanganyika

Nazungumzia Uhuru wa Tanganyika. Sizungumziii Uhuru wa Tanzania Bara.

Majuzi niliona mabango yaliyosambazwa jijini Dar es Salaam. Mabango hayo yalisomeka “SHEREHE ZA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA BARA”.

Read More »

Zuma: Nelson Mandela amepumzika kwa amani

Alhamisi usiku Desemba 5 mwaka huu, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini,  alitangaza kifo cha Rais wa kwanza mweusi nchini humo, Nelson Mandela, ambaye amefariki dunia  akiwa na umri wa miaka 95.

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons