Changamoto za majina maarufu

Kwenye Mkutano wa 18 wa Bunge uliopita, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) aliongea bungeni na kuhoji uamuzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutumia wasanii Watanzania kutangaza vivutio vya utalii nchini. Mchungaji Msigwa alisema kuwa wasanii hao hawajulikani na ingefaa kutumia wasanii wa nje wanaofahamika zaidi. Katika kusisitiza hoja yake, alimtaja msanii…

Read More

Jifunze kushukuru katika maisha (1)

“Shukrani ni fedha ambayo tunaweza kujitengenezea sisi wenyewe na kuitumia bila kuogopa kufilisika.” – Fred De Witt Van Amburgh Siku moja kipofu alikuwa anasafiri. Akakutana na barabara mbaya sana. Akasimama akawaza sana. Akajiuliza nitawezaje kusafiri katika barabara mbovu kiasi hiki wakati sioni?  Pembeni ya barabara kulikuwa na mlemavu ambaye naye alikuwa anataka kusafiri. Kipofu alisimama…

Read More

Bado Muhandiki ni mhimili wa ushirika

Yamesemwa mengi baada ya mzee Arhard Felician Muhandiki kukatwa mguu kutokana na maradhi yaliyompata.  Kuna baadhi ya watu walifurahia sana tukio hilo wakidhani kuwa hiyo itakuwa nafuu kwao kwa jinsi alivyokuwa amewakalia kooni katika walichokiona kama fursa kwao. Kwa muda mrefu Muhandiki alijitoa kama mpambanaji wa kunusuru mali ya ushirika iliyokuwa ikipotea kama mali isiyokuwa…

Read More

Sijajua Watanzania tunachotaka

Mwalimu Julius Nyerere aliamini katika dhana ya maendeleo ya watu, na si maendeleo ya vitu. Dhana hii imepewa tafsiri nyingi. Wapo wanaoamini kuwa Mwalimu hakutaka kuona barabara, majengo makubwa makubwa na miradi mingine yenye thamani ya mabilioni ya fedha. Lakini ukirejea kwenye matendo ya Mwalimu unakutana na vielelezo vinavyokinzana na hao wanaojaribu kuupindisha ukweli wa…

Read More

Vijana ni wajenzi, wachafuzi wa nchi

Vijana ni nguvu kazi na viongozi wa taifa lolote duniani. Ni walinzi na wana utamaduni wa nchi yoyote duniani. Sifa ambazo wanazo tangu zama hadi sasa. Lakini kihistoria na kisiasa inaeleweka wajenzi wakubwa wa dunia ni vijana na wachafuzi wakubwa wa dunia ni vijana. Sifa zote hizi ni zao. Vijana wanatambulika na wanaaminika wanayo mawazo…

Read More