Moshi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimejitosa kusimamisha mgombea jimbo la Siha, kuchuana na mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel.
Dk Mollel alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema
hadi Desemba 14 mwaka jana, alipojivua uanachama Chadema na kujiuzulu ubunge ili kumuunga mkono Rais John Magufuli.

Taarifa zilizothibitishwa na uongozi wa chama hicho,zilisema kamati ya utendaji ya Wilaya ya Siha iliyoketi juzi imefanya uteuzi wa awali na kumteua Elvis Mossi kugombea ubunge jimbo la Siha.

Hata hivyo, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema mbali na kuthibitisha taarifa hizo leo Alhamisi, lakini amesema uteuzi huo wa Mossi utasubiri baraka za Kamati Kuu ya Chadema.

“Kilichofanyika ni uteuzi tu wa awali kamati kuu ikishatoa kukubali, kukataa au hata kubadilisha mgombea,”amesema kuzungumzia uteuzi huo akisema anaweza kufanya hivyo baada ya Kamati Kuu kuridhia uteuzi huo na kwa sasa itakuwa mapema kuuzungumzia”.

1431 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!