Meshack Turento

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara, Meshack Turento ametangaza kujivua wadhifa huo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi akidai chama hicho (CHADEMA) imewatelekeza.

Akizungumza jijini Arusha Turento alidai kuwa, kabla ya kujiunga na CHADEMA alikuwa mwanachama wa CCM, lakini baadae aliona chama hicho kimepoteza mwelekeo na kujiunga na CHADEMA, ila sasa ameamua kurejea CCM baada ya kuona ndani ya CCM kuna mabadiliko makubwa.

 

Pia alisema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM taifa kwa kuimarisha chama hicho na kukijengea mfumo mzuri wa madaraka

 

Hata hivyo alikanusha taarifa za yeye kutishwa kukamatiwà mifugo yake iwapo ataendelea kubaki CHADEMA na kudai si za kweli na wala hajanunuliwa.

 

1536 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!