MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi.

Samia amtembelea Lissu baada ya kumalizika kwa hafla ya kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Mhe. Samia Suluhu Hassan alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

By Jamhuri