KOREA KASKAZINI YAFUNGUA MAWASILIANO YA SIMU NA KOREA KUSINI

Korea Kaskazini imefungua tena mawasiliano ya simu na Korea Kusini ili kuanzisha mazungumzo kuhusu kushiriki kwake katika mashindano ya msimu wa baridi.

Korea Kusini imethibitisha kuwa ilipata simu kutoka Kaskazini leo Jumatano.

Hii ni baada ya Kim Jong un kusema kuwa ataanzisha mazungumzo na Korea Kusini kuhusu kutumwa timu kwa mashindano ya msimu wa baridi huko Korea Kusini.

Mataifa hayo mawili hayajafanya mazungumzo ya juu tangu Disemba mwaka 2015

Mwaka uliofuatia Korea Kaskazini ilikata mawasiliano na kuacha kupokea simu kwa mujibu wa maafisa kutoka Kusini

Afisa kutoka Korea Kaskazini alitangaza kufunguliwa laini hiyo ya simu kwenye ujumbe uliopeperushwa mapema Jumatano.

Mkuu wa idara ya mawasiliano ya raia wa Korea Kusini Moon Jae-in, alisema kuwa kufunguliwa kwa laoni hiyo ya simu kuna umuhimu mkubwa

“Inabuni mazingira ambapo mawasiliano yatakuwa rahisi kila mara,” alisema.

 

Source: BBC Swahili.