Mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa kisiasa na askari polisi wamejitokeza kuuaga mwili wa mke wa Naibu waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Kangi Lugola, Bi Marry Lugola Jijini Dar es salaam.

Bi Marry Lugola ambaye alikuwa Kamishna Msaidizi wa polisi amegwa hii leo nyumbani kwake Railywa Gerezani Jijini Dar es salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mwibara, Bunda kwa Mazishi.

Akieleza maisha ya Mke wake Mh Lugola amesema, yeye na familia yake wamempoteza mtu muhimu katika familia hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba ameiwakilisha serikali katika mazishi hayo na hapa anatoa salamu za serikali.

Marehemu Marry Lugola amefariki dunia January mosi mwaka huu baada ya kusumbuliwa na shinikizo la Damu.

Katika hatua nyingine MWILI wa  aliyekuwa mpigapicha wa magazeti ya serikali (TSN), Athumani Hamisi Msengi,  unatarajiwa  kuzikwa  kesho Januari 5 mchana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Marehemu amefariki dunia asubuhi  leo katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili alikofikishwa kwa matibabu baada ya  kuzidiwa ghafla usiku akiwa nyumbani kwake sinza Jijini Dar es salaam.

1741 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!