LISOME GAZETI LETU LA JAMHURI LA KILA WIKI HAPA

Habari Mpya

Dk. Lwaitama: Serikali tatu hazikwepeki

 

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azavel Lwaitama (pichani), amesema suluhisho pekee la kunusuru Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuwa na Serikali tatu.

Dk. Lwaitama alitoa kauli hiyo katika Mazungumzo ya Asubuhi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania na kufanyika katika Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam jana.

Read More »

Serikali yaelekea kukubali hoja ya Waislamu

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inaelekea kulikubali ombi la kundi la waumini wa Kiislamu wanaotaka dodoso la dini liingizwe kwenye Sensa ya Watu na Makazi iliyopangwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu.

Uamuzi huo ambao umeshawahi kupingwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk. Albina Chuwa, unatajwa kwamba huenda ukatangazwa hivi karibuni baada ya ngazi ya juu ya uongozi “kutafakari” na kubaini kuwa dodoso hilo haliwezi kuathiri umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Read More »

Biashara za sasa zinahitaji u-sasa

Ingawa kuna mambo mengi hapa katika u-kisasa, kwa leo nitagusia maeneo matatu tu. Mosi, kuweka biashara katika mifumo rasmi; pili kuwa na maono; na tatu kutengeneza mfumo wa kurithisha biashara kutoka baba kwenda kwa watoto - kutoka kwa wajukuu kwenda kizazi cha pili. Biashara katika mifumo rasmi ina dhana pana, lakini kwa urahisi kabisa ni kuendesha biashara katika mifumo inayoelezeka. Ni ile hali ambayo mmiliki unapokuwapo au kutokuwapo biashara inaendelea kama kawaida.

Read More »

Niliyojifunza ufunguzi wa Olimpiki

JIJI hili sasa hivi hakuna kingine kinachozugumzwa wala kusikilizwa kupita michezo ya Olimpiki. Nimekubali kwamba ni michezo mikubwa na faida yake kwa waandaaaji si ndogo.

Ukishaona watu wanafanya kampeni kubwa kama Uingereza ili tu waandae kitu hiki kwa mara ya tatu, lazima ujue kuna manufaa.

Read More »

Hotuba iliyowazima  wabunge mafisad

Bunge linanuka rushwa. Baadhi ya wabunge wanapokea rushwa ili kutetea maslahi ya wanaowatuma. Lakini wapo wabunge jasiri walioamua kupambana na wenzao wala rushwa kama inavyothibitishwa ...

Read More »

Bahanuzi aleta ladha katika soka

LICHA ya Tanzania kumudu kulibakiza nyumbani Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati – maarufu zaidi kwa jina la Kagame – mshambuliaji wa Simba Sports Club, Felix Mumba Sunzu ameibuka kuwa galasa huku mashabiki wakijiuliza kuhusu sifa zinazofanya timu hiyo iendelee kumng’ang’ania.

Read More »

Muhongo, Maswi wanatisha

 

*Gharama za kuunganisha umeme zakuna wengi

*Migodi yote si hiari tena kulipa kodi ya mapato

*Afuta mashangingi ya bure, vigogo watakopeshwa

*Mnyika, Selasini wawanyoosha wabunge wala rushwa

 

Wananchi wengi wameeleza kufurahishwa na msimamo wa uongozi mpya wa Wizara ya Nishati na Madini wa kuwapunguzia wananchi ukali wa gharama za kuunganisha umeme, kufuta ununuzi wa mashangingi na kuwabana wenye migodi mikubwa kuanza kulipa kodi ya mapato.

 

Read More »

Haya ndiyo mambo murua yanayoliliwa na Watanzania

Wizara ya Nishati na Madini imetangaza kupunguza gharama za kuunganishia wateja wake umeme. Gharama hizo zimepungua kwa wastani wa asilimia 30 na 77. Uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, bungeni mwishoni mwa wiki.

Read More »

Biashara za sasa zinahitaji u-sasa

Wakati baba yangu mzazi akifariki katikati ya miaka ya 1990, alikuwa mmoja wa wafanyabiashara waliokuwa wakipanda kwa kasi kubwa kibiashara. Akiwa ameshakusanya uzoefu wa kusafiri kibiashara hadi nchi jirani ikiwamo Malawi, alifariki dunia na kuacha biashara zilizokuwa zimestawi kweli kweli.

Read More »

Habari za Kitaifa

Maoni ya Mhariri

Nyundo ya Wiki