Category: Kimataifa
Rais wa kwanza wa Namibia afariki akiwa na umri wa miaka 95
Rais wa kwanza wa Namibia huru, Sam Nujoma, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 katika mji mkuu wa Windhoek, kiongozi wa sasa wa nchi hiyo ametangaza. Nujoma aliongoza vita vya muda mrefu vya kudai uhuru kutoka kwa Afrika…
Watu 30 hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi China
Takribani watu 30 wametangazwa kuwa hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Jinping kilichopo kusini-magharibi mwa China, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya China. Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea katika kijiji cha Jinping kilichopo…
Trump apiga marufuku wanamichezo wa kike waliobadili jinsia kushindana mashindano ya wanawake
Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini agizo linalozuia wanawake waliobadili jinsia kushindana katika michezo ya wanawake. “Kuanzia sasa, michezo ya wanawake itakuwa ya wanawake tu,” Trump alisema, akizungukwa na wanariadha wanawake na wasichana kabla ya kusaini agizo hilo huko…
Prince Rahim Al-Hussaini ateuliwa kuwa Aga Khan mpya
Prince Rahim Al-Hussaini ametangazwa kuwa Aga Khan mpya, kiongozi wa kiroho wa mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ya Ismailia. Atachukua nafasi hiyo kutoka kwa babake Prince Karim Aga Khan, aliyefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 88. Uteuzi…
DRC: Tangazo la M23 la usitishaji vita sio la kuaminika
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeelezea hatua ya kusitishwa mapigano iliyotangazwa na waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo kama “mawasiliano ya uongo.” Kulingana na msemaji wa serikali ya Kongo Patrick Muyaya, wanachosubiri kwa sasa ni kuondoka nchini…
Shirika la Posta la Marekani lasimamisha usafirishaji mizigo ya China
Shirika la Posta la Marekani limesema limeacha kupokea mizigo kutoka China bara na Hong Kong kwa muda usiojulikana. Huduma ya barua haitaathiriwa na usitishaji huo, ilisema shirika hilo, ambalo lilikataa kutoa sababu ya uamuzi huo. Hata hivyo, mnamo Jumanne sheria…





