JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Weah: Mwanasoka aliyetamba dimbani, akatikisa katika siasa

Baada ya kumalizika kwa vita ya muda mrefu ya wenyewe kwa wenyewe huko Liberia, mwanasoka mstaafu, George Opong Weah, alitangaza kuwania urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, kisha akaanzisha chama kinachoitwa Congress for Democratic Change (CDC).

Tuwafundishe wasomi wetu kujiajiri

 

Miezi ya karibuni kule nchini Marekani askari walipambana na waandamanaji waliokuwa wakilalamika kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho.

 

Mara kadhaa waandamanaji hao wamejaribu kuandamana kupitia njia mbalimbali, ikiwamo ile ya kukutana kwenye daraja la Mto Mississipi lakini mara zote wameambulia kufurumushwa na polisi.

 

Kashfa ya riba na vituko vya binti wa mkurugenzi

London ina upepo, ubaridi wa haja na mvua kwa siku mbili tatu hizi, lakini kuna wanaotokwa na jasho. Kihoro kimewashika wanene wachache, kwa sababu ya kashfa ya kupanga viwango vya riba za kukopeshana kwa benki za hapa.

Brigedia Jenerali Aliasa Taifa

*Asema udini na ukabila ni ufa unaobomoa Taifa letu

 

Moja ya hotuba za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, zisizochujuka ni ile aliyoitoa pale Kilimanjaro Hotel mbele ya Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania Machi 13, 1995.

 

Katika mazungumzo yake siku ile alitaja nyufa tano zinazolitikisa  Taifa letu kuanzia kwenye paa, katika dari, kutani hadi kufikia katika msingi ule imara wa Taifa uliojengwa kwa muda mrefu. Nyufa zilizotajwa zilikuwa:-

 

* Muungano

* Kupuuza na kutojali

* Kuendesha mambo bila kujali sheria

* Rushwa, na

* Ukabila na udini.

 

Mchechu NHC ameonyesha njia, wakurugenzi wengine mko wapi?

Wiki iliyopita Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limepata mkopo wa wastani wa Sh bilioni 165. Shirika limeupata mkopo huu kutoka benki na mashirika tisa ya fedha. Mashirika na benki zilizotoa mkopo huu na kiasi cha fedha walizotoa kwenye mabano ni CRDB Bank (Sh 35 bilioni), ECO Bank (Sh 20 bilioni), ABC (Sh 4 bilioni), NMB (Sh 26 bilioni), CBA (Sh 24 bilioni), TIB (Sh 22 bilioni), Azania (Sh 7 bilioni), Local Authorities Pension Fund-LAPF (Sh 15 bilioni) na Shelter Africa Company (Sh 22 bilioni).

 

Dk. Ulimboka siri zavuja

*Uchunguzi waanza kuleta majibu yenye utata
*Yadaiwa madaktari walimshitukia, wakamteka
*Madaktari wasisitiza serikali haiwezi kujinasua

Siri za uchunguzi wa awali wa tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk. Stephen Ulimboka zimeanza kuvunja, lakini kwa mshangao wa wanaojua kilichotokea, uchunguzi huo unatoa majibu yenye tata.