Latest Posts
NUKUU ZA WIKI
Mwalimu Nyerere: Wanadamu huongozwa na sheria
“Nchi zote duniani huongozwa na wanadamu na si malaika. Wanadamu hawa huongozwa na sheria na si kwa akili zao wenyewe.”
Haya ni maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius K. nyerere.
Tuhuma za ujangili: Mtutura awashukia wabaya wake, Kamanda Tossi
Wiki mbili zilizopita, Gazeti hili liliandika habari zinazohusu kukamatwa kwa msaidizi wa Mbunge wa Tunduru Kusini, Mtutura Mtutura, akiwa na bunduki za mbunge huyo zinazohusishwa kwenye matukio ya ujangili. Baada ya taarifa hiyo, Mtutura amejitokeza kukiri kukamatwa kwa bunduki hizo na ukweli wa mambo ulivyokuwa. Ifuatayo ni kauli ya mbunge huyo tunayoichapisha bila kuihariri.
Julio: Kibadeni atafanya makubwa Simba
Kocha Msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club ya Dar es Salaam, Jumhuri Kiwelu ‘Julio’ amesema kuwa kuwapo kwa Kocha Mkuu mzawa katika timu hiyo, King Abdallah Kibadeni ‘Mputa’, kutaiwezesha kufanya vizuri katika michuano ijao.
vVyombo vya dola visimchekee polisi huyu
Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi lilimtia mbaroni mmoja wa askari wake, baada ya kumkuta akiwa na risasi 200 ambazo haijajulikana alikotaka kuzipeleka.
Polisi matatani tena
JESHI la Polisi limeingia matatani kwa kumtangaza ‘mbaya wao’ aliyeibua kile alichodai kwamba ni mtandao wa uhalifu na mauaji ndani ya Jeshi hilo mkoani Mwanza, kwamba ni kichaa.
Misitu ya Asili na Maendeleo ya Jamii Tanzania (1)
Kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na dunia na vyote vilivyomo tukiwamo sisi wanadamu, kwa mema mengi mno anayonitendea na hasa kwa kutujalia uhai hadi leo hii.