Daily Archives: April 24, 2019

CUF njia panda

Wabunge 24 wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye amehamia Chama cha ACT – Wazalendo, wataendelea kushikilia ubunge wao hali inayoiweka CUF njia panda, JAMHURI limeelezwa. Wabunge hao walijikuta katika mtihani wa kuchagua ama kuachana na ubunge wao wamfuate Maalim Seif ACT au wabaki CUF kulinda ubunge wao hadi ...

Read More »

Neno la Pasaka kutoka kwa Askofu Bagonza

IJUMAA KUU – KANISA KUU LUKAJANGE 2019 MATHAYO 27: 27-31, 39-40 “Ndipo askari wa Liwali wakamchukua Yesu ndani ya Proitorio,* wakamkusanyikia kikosi kizima. Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu. Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhiaki, wakisema: ‘Salaam, Mfalme wa Wayahudi!’ Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, ...

Read More »

Ujenzi Ziwa Victoria wazua jambo

Mradi mkubwa wa maji unaojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) umeingia lawamani baada ya kampuni inayojenga kuanza kumwaga vifusi vya udongo ndani ya Ziwa Victoria. Hali hiyo inayodaiwa kusababisha uchafuzi wa mazingira, inalenga kujenga barabara ya udongo ziwani ambayo itarahisisha ufungwaji wa mitambo ya kusambaza maji ya kunywa kwa wananchi. Taarifa zinabainisha hadi sasa zaidi ya ...

Read More »

Bodi ya Ngorongoro isifumbiwe macho

Miongoni mwa habari tulizozipa umuhimu wa juu hivi karibuni ni ile inayohusu matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlala ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amebaini kuwa kwa mwaka uliopita, bodi hiyo iliketi vikao 20 badala ya vikao vinne vya lazima na viwili vya kazi za ukaguzi na ...

Read More »

NINA NDOTO (16)

Kuwa na nidhamu utimize ndoto yako Kama yalivyo muhimu mafuta kwenye gari, ndivyo ilivyo nidhamu kwa mtu yeyote mwenye ndoto. Nidhamu ni kiungo muhimu kwa mtu anayetaka kutimiza ndoto yake. Kuna aliyesema: “Nidhamu ni msingi wa maisha yenye furaha na mafanikio.” Ni wazi kuwa umesikia watu wengi wakitaja siri za mafanikio neno ‘nidhamu’ huwa halikosi. Vitu vinavyowafanya watu wengi wafanikiwe ni ...

Read More »

Shamba la Lyamungo mali ya KNCU – Waziri

Mvutano unaoendelea kuhusu nani mmiliki halali wa shamba la kahawa la Lyamungo baina ya Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) na Chama cha Ushirika wa Mazao (AMCOS) cha Lyamungo unatokana na Ofisi ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kutochukua hatua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba suala hilo lilikwisha kuamuliwa miaka 14 iliyopita na aliyekuwa Waziri wa Ushirika ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (11)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kusema kuwa leo nitaelezea masharti na aina ya viambatanisho unavyopaswa kuweka katika kuwasilisha fomu ya maombi ya leseni. Naomba kuwashukuru wasomaji wangu kwa kunipigia simu nyingi kadiri inavyowezekana na kwa kuonyesha kuwa mnatamani kupata kitabu hiki haraka kadiri inavyowezekana. Sitanii, kitabu hiki nitakichapisha na kukiingiza mitaani hivi karibuni, ila nawaomba uvumilivu. Wapo mliotaka niwatumie ...

Read More »

Hatua kubwa miaka 55 ya Muungano

Aprili 26, mwaka huu taifa litaadhimisha miaka 55 tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Umri huo wa miaka 55 ya Muungano si haba, changamoto na mafanikio kadhaa yamekwisha kujidhihirisha na kubwa zaidi kwa upande wa mafanikio kuimarika kwa mshikamano baina ya raia wa pande hizo mbili za Muungano. Serikali zote mbili, yaani ...

Read More »

Funzo miaka 25 mauaji ya Rwanda

Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yametimiza miaka 25. Huu ni umri wa mtu mzima na hili linajionyesha wazi kule Rwanda, asilimia 60 ya watu wa Rwanda ni vijana na wengi wao ni miaka 25 na kwenda chini. Wengi wamezaliwa baada ya mauaji haya ya kinyama. Aprili 7, 2019 Rwanda ilifungua siku mia moja za maombolezo ya kumbukumbu ya miaka 25 ...

Read More »

UJENZI GATI JIPYA LA MAGARI BANDARI YA DAR WAFIKIA ASILIMIA 50

Kazi ya utekelezaji wa ujenzi wa Gati mpya kwa ajili ya kuhudumia Meli za magari (RoRo Berth) kwenye Bandari ya Dar es Salaam imefikia asilimia 50 na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019. Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema mbali na kukamilika kwa ujenzi wa Gati hiyo unaotarajiwa kukamilika katikati ya 2019, kazi ya kuboresha Gati namba ...

Read More »

Watanzania tunaepushwa mengi

Matukio ya hivi karibuni ya nchini Sudan yanatukumbusha umuhimu mkubwa wa dhana ya kung’atuka, neno la Kizanaki lililoingia kwenye msamiati wa lugha ya Kiswahili na ambalo husikika pia kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Raia wa Sudan wamekuwa kwenye kipindi cha miezi kadhaa ya maandamano ya kushinikiza serikali yao kuachia madaraka na kuanzisha mchakato wa kurudisha utawala wa kiraia. Maandamano ...

Read More »

Haki za mtuhumiwa mbele ya polisi

Mtuhumiwa ni nani? Ni mtu yeyote anayewekwa chini ya ulinzi na polisi au chombo cha usalama kwa kutuhumiwa kufanya kosa la jinai. Makosa ya jinai ni yapi? Ni makosa ambayo mtu akipatikana na hatia hupewa adhabu. Ni makosa kama wizi, ubakaji, mauaji, kufanya makosa ya kuhatarisha amani na mengine ya namna hiyo. Haki za mtuhumiwa Mtuhumiwa anapowekwa chini ya ulinzi ...

Read More »

Ndugu Rais maneno makali ni maneno gani hayo?

Ndugu Rais, wapo wanaosema kuna maneno ambayo ni makali. Ni yapi hayo maneno makali? Ukali wake upo kwa namna yanavyotamkwa kwa ukali au ukali wake uko katika maneno yenyewe kuwa hata ukiyatamka kwa upole yanabaki kuwa makali? Kwamba, hata yakiwa yenyewe kama ni kitabuni au wapi yanakuwa makali. Maneno makali ni yapi? Ukimwambia timamu ambaye si dhaifu kuwa ni dhaifu, ...

Read More »

Epuka kuishi maisha ya majivuno (3)

Fumbua macho yako utazame. Tazama upya uhusiano wako na Mungu wako. Tazama upya uhusiano wako na mke/mume wako. Tazama upya uhusiano wako na watoto wako. Tazama upya uhusiano wako na majirani zako. Tazama upya uhusiano wako na kazi yako. Tazama upya uhusiano wako na wafanyakazi wenzako. Baada ya kutazama umebaini nini? Je, umebaini kasoro za kiuhusiano? Jifunze kumwomba msamaha aliyekukosea ...

Read More »

Kupenda si kazi, kazi ni kumpata akupendaye

Kupendwa ni mtihani.  Kupenda ni kujiweka katika hatari ya kutopendwa. Lakini hatari kubwa ni kutojiweka katika hatari. Kupenda si kazi, kazi ni kumpata akupendaye. Kuna methali ya Wahaya isemayo: “Mwereka wa mzazi unaomwangukia mtoto, si mwereka wa mtoto unaomwangukia mzazi.” Mzazi anajitaabisha kukidhi mahitaji ya mtoto, lakini baadaye mtoto hajitaabishi kukidhi mahitaji ya mzazi. Kwa msingi huu kupendwa ni mtihani. ...

Read More »

Uhuru una kanuni na taratibu zake

Uhuru ni uwezo au haki aliyonayo mtu binafsi, jumuiya au taifa ya kujiamulia mambo yake kwa hiari yake bila kuingiliwa na mtu au taifa jingine. Kuna uhuru wa mtu binafsi, ambao humpa haki ya kuishi akiheshimika sawa na watu wengine. Mtu binafsi huwa na haki ya kutoa mawazo yake, kufuata dini anayoipenda na kushiriki katika uamuzi wa mambo yote yanayohusu ...

Read More »

Yah: Mkuu, huku mbwa atamla mbwa

Kama siku zote ninavyosema salamu ni ada, na ni uungwana kujuliana hali, nawashukuru sana wote wanaonitumia ujumbe wa simu kunieleza yale ambayo yamewakuna. Hata kama litakuwa si jema kwako, naomba unijulishe ili nijue kuwa nimekukera, sisi ni binadamu, hiyo ni hatua ya maisha na lazima niipitie ili niweze kukiri, hakuna binadamu mkamilifu, karibu wote ni dhaifu. Kuimaliza wiki ukiwa salama ...

Read More »

Bodi ya Ligi gumzo

Hali ya soka nchini hususan mwenendo wa michezo ya ligi kuu si ya kuridhisha. Kumekuwa na lawama kutoka kwa wadau wa soka zinazoelekezwa kwa waamuzi wa mechi mbalimbali, lakini kwa upande mwingine, vilevile kumekuwa na malalamiko dhidi ya Bodi ya Ligi Tanzania Bara. Wakati waamuzi wakilalamikiwa  kutokuwa imara na makini katika baadhi ya mechi wanazosimamia, Bodi ya Ligi imekuwa ikishutumiwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons