Ya AFCON, Taifa Stars na maagizo ya Rais Yoweri Museveni
Ukitaka kufahamu habari za mjini – mji wowote – muulize dereva wa teksi. Kwa kawaida ana taarifa nyingi na muhimu, na si ajabu kuwa hivyo. Anabeba abiria kila wakati na abiria kama ilivyo tabia ya binadamu yeyote, wana mdomo na hushindwa kukaa kimya kwa muda mrefu. Lazima watakuwa na kitu wanakiwaza na mawazo yanapozidi huyamwaga….