Marufuku ya matumizi ya adhana{ Wito kwa Waislamu kuhudhuria maombi} katika tarafa moja ya mji wa Kigali nchini Rwanda imepingwa vikali na baadhi ya Waislamu jijini humo.

Utawala katika tarafa ya Nyarugenge kunakopatikana jamii kubwa ya Waislam nchini humo umebainisha kuwa kumekuwepo muafaka wa kubadili mbinu za kuwaita waumini bila ya matumizi ya njia hiyo ambayo inatajwa kuwasumbua wananchi.

Kulingana na taarifa kutoka Kigali Waislamu kuhudhuria maombi umetajwa kuwa kero miongoni mwa wananchi.

Tayari mkataba wa kuhakikisha kuwa mwafaka huo unaheshimiwa umetiwa saini kati ya viongozi wa msikiti na utawala wa eneo hilo.

Wito huo wa maombi miongoni mwa jamii za Waislamu kote duniani hutumia vipaza sauti na hufanyika mara tano kwa siku.

Licha ya utawala wa eneo hilo kudai kwamba kumekuwa na mwafaka kutoka pande zote mbili baadhi ya Waislamu waliohojiwa wametoa hisia tofauti.

Kulingana na katibu mtendaji wa tarafa hiyo ya Nyarugenge, amri hiyo iliagizwa yapata miaka maiwili iliopita lakini ikapuuziliwa mbali.

”Pengine wakati ule sababu ambazo watu hawakupokea vyema ujumbe ilikuwa hakuwa umeelezewa sawa sawa ,lakini leo baadhi ya makanisa yalilazimika kufunga milango baada ya kushindwa kutimiza kanuni za ujenzi huku misikiti yenye vipaza sauti na makanisa yenye kengele tukiyataka kutotumia mtindo huo. Mtu aliye lala akiishi jirani na kengele hiyo inampigia kelele. Kwa hiyo ni uamzi unaohusu pande zote nna ni matarajio yetu kuwa hakuna aliyenyimwa haki.”

Naye mshauri wa Mufti wa Rwanda shekh Mbarushimana Suleinam alisema kuwa hatua hii ya kuzuiliwa kwa matumizi ya adhana misikiti inafuatia operesheni inayoendela ya kufungwa kwa makanisa na vigango Zaidi ya mia saba ambavyo viliripotiwa kuwa havijatimiza kanuni za ujenzi na amri ilitolewa kwanza kutimiza matakwa ili zipewe tena idhini ya kufanya kazi.

 

By Jamhuri