Staa wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’ (kushoto) akiwa na mcheza soka aliyeko Afrika Kusini,  Uhuru Selemani, wakiongea na wanahabari leo Uwanja wa Taifa, Dar.

 

MKALI wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba  ‘Alikiba’,  amemuonya mwanasoka  mshambuliaji wa klabu ya Ubelgiji ya  KRC Genk, Mbwana Samatta,  kwamba ataondoka uwanjani analia watakapokutana Jumamosi katika mchezo maalum wa kuchangia elimu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Timu ya Alikiba na timu ya Samatta, zitapambana kwenye uwanja huo Jumamosi wiki hii katika mchezo huo uliodhaminiwa na Kampuni ya Asas.

Alikiba na  Uhuru Selemani wakionyesha moja ya majezi ya mchezo huo.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa atahakikisha mpinzani wake anaondoka akiwa analia kutokana na kuchagua kikosi bora kwa ajili ya mchezo huo utakaowajumuisha wachezaji wengi wa kimataifa.

“Nitahakikisha Samatta anaondoka analia kwani kikosi changu kipo vizuri nikiwa na wachezaji wanaocheza ndani na nje ya Tanzania, kwani tunaye Uhuru Selemani ambaye naamini kwa ushirikiano wake na wengine tutapata matokeo mazuri,” amesema Alikiba.

2474 Total Views 1 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!