Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bw. Ramadhani Musa Khijjah (65), amefariki dunia alfajiri ya kuamkia Aprili 17 katika eneo la Jet Lumo, wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam.

Maziko yatafanyika leo Aprili 18, katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, saa 10 jioni.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu Ramadhan Khijjah katika eneo la Jet Lumo, Yombo Malawi Hospital-Temeke.

Marehemu Ramadhani Khijjah aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali wakati huo Wizara ikijulikana kama Wizara ya Fedha na Uchumi, Novemba 23, mwaka 2008.

Alistaafu utumishi wa umma mnamo na June 12, 2013 akiwa na umri wa miaka 60.

Wakati wa uhai wake, Marehemu Khijjah, atakumbukwa kwa uchapakazi wake hodari, uadilifu, uzalendo na alichukia vitendo vya rushwa,.

Imetolewa na

Benny Mwaipaja

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Fedha na Mipango

 

By Jamhuri