Baada ya kuthibitisha rasmi kuwa watashiriki michuano ya KAGAME CUP inayotaraji kuanza Juni 28 2018, uongozi wa klabu ya APR umeomba kubalidishwa ratiba.

Hatua hii imekuja mara baada ya CECAFA kuwapangia APR kucheza na Singida United Juni 29 itakayokuwa Ijumaa ya wiki lijalo.

Taarifa kutoka Rwanda zinaeleza kuwa APR wamesema uchovu wa safari kwa wachezaji wao unaweza ukachangia wasioneshe kiwango kizuri hivyo ni vema wakapata muda kidogo wa kupumzika.

Kutokana na tarehe 29 iliyopangwa, viongozi wa klabu hiyo wameomba iwe siku tofauti, ikiwezekana isogezwe mbele.

Ikumbukwe APR walipewa mwaliko wa kushiriki mashindano haya kutokana na baadhi ya timu kujiondoa kwa madai ya kuwa hayakuwa yanaendana na ratiba.

Tayari Singida nao wamethibitisha kupokea barua ya CECAFA jana na wamesema wako tayari kushiriki na wanaisubiri APR kwenye mchezo wao wa kwanza.

 

1531 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!