Kundi la wanaharakati lenye wafuasi zaidi ya elfu arobaini kutoka visiwani Zanzibar wamefungua kesi katika mahamaka ya Afrika Mashariki wakitaka Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar uvunjwe kwa madai kwamba hauna uhalali. Rashid Salum Adiy ambae ni mmoja wa wanaharakati waliofungua kesi hiyo, amesema kwamba, wamekwenda katika mahakama hiyo ya Afrika Mashariki baada ya mahakama kuu Zanzibar kushindwa kuisikiliza kesi hiyo.

 

SOURCE: BBC SWAHILI

1950 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!