Peter ambaye ni baba mzanzi wa Peter Manyika, amefunguka kuhusiana na sakata la mtoto wake kujiengua kwenye timu ya Singida United akieleza kutolipwa stahiki zake.

Peter amesema kuwa ni kweli mtoto wake ameshaondoka SIngida na sasa yupo katika kituo cha soka anachokimiliki jijini Dar es Salaam akijifua kulinda kiwango chake.

Mzee huyo ameeleza kuwa ni kweli Singida hawajamlipa stahiki zake ikiwemo fedha za usajili pamoja na mshahara wa miezi kadhaa jambo ambalo limepelekea mwanaye kujiondoa kambini.

Kwa mujibu wa Radio One, Peter ameeleza kuwa Singida wamekuwa wakifanya mazungumzo naye kwa ajili ya kumalizana na Manyika Jr ili aweze kurejea kikosini.

Singida wamekuwa wakimtumia Peter ili kurahisisha njia ya kumrudisha kipa huyo aweze kuendelea na majukumu ya kuitumikia klabu kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi chao.

Kipa huyo alisajiliwa na Singida United baada ya msimu wa 2016/17 kumalizika akiwa huru.

1030 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!