Barua yangu kwa Profesa Ndalichako (2)

Sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii, mwandishi alisema ni vyema serikali ikashauriwa juu ya hatari  iliyo mbele yetu ya elimu inayotolewa sasa kama haitachukuliwa mikakati ya dhati na makusudi ili  kuibadilisha na kuirudisha katika hali ya elimu ya Serikali ya Awamu ya Kwanza.

Akasema hili linawezekana tu kama kutakuwa na utashi wa dhati kwa kisiasa kutoka kwa viongozi wa Serikali, hasa Wizara ya Elimu. ENDELEA…

 

Hivi sasa Wizara ya Elimu imetoa sera mpya ya elimu. Ili kuhakikisha  fursa za elimu na mafunzo zinapatikana kwa kila Mtanzania  bila ubaguzi wa jinsi, rangi, kabila, dini, ulemavu na hali ya kijamii na kipato,  ninapendekeza kuongeza matamko yafutayo katika masuala ya sera  mpya ya elimu  kama ifutavyo:

 

 Suala

Upimaji, tathimini na maendeleo ya wafanyakazi katika elimu na mafunzo-uk.38

Napendekeza kuongeza tamko lifuatalo ili kuboresha utekelezaji wa suala hili.

3.2.23 Serikali iondoe utungaji wa mitihani ya kuchagua maswali (multiple choice) na kutunga maswali ya kujieleza. Kwa mfano swali katika somo la fizikia liwe katika mfumo ufutao:

 

SWALI NA.I

· What is potential energy

· Explain at least two uses of potential energy in daily life.

· Find the potential Energy gained by a 1300 g box lifted at 1200m.

 

Mwanafunzi ajibu maswali Na. (a) na (b) kwa kujieleza na kuonyesha njia jinsi alivyopata jibu la swali Na.(c)

 

Maelezo: Ni kupima na kupanua uelewa wa mwanafunzi katika somo husika.  Maswali ya kuchagua, hata kama mwanafunzi hauji kuna uwezekano mwanafunzi kufaulu kwa kubahatisha tu.

 

Suala

Fursa kwa usawa katika elimu na mafunzo-uk.40

Ili kufanikisha azima hii, napendekeza kuongeza   tamko (uk.41) lifuatayo wenye suala hili:

3.3.3 Muhtasri (syllabus) ifundishwe ya aina moja kwa shule zote za Serikali na binafsi ikiwa ni pamoja na lugha ya kufundishia.

 Maelezo: Kama ikiendelea kama ilivyo sasa,  fursa hii baina ya wanafunzi wanaosoma shule za Serikali ambao idadi yao kubwa ni watoto wa Watanzania maskini na shule binafsi ambao idadi yao ni watoto wa wenye uwezo (wafanyakazi, wanasiasa, wafanyabiashara na viongozi wa madhehebu ya dini) haitakuwapo, ambako si lengo la suala hili.

 

Suala

Ugharimiaji elimu na mafunzo nchini-uk 55

Ili mfumo huu uwe endelevu, napendekeza kuongeza matamko yafutayo:

3.6.3 Makundi yafuatayo ambayo yanapata mapato yao kwa kufanya kazi serikalini au kufanya kazi na Serikali, watoto wao wasome katika shule za Serikali. Utaratibu huu, uanze mwaka 2017.

i)Wafanyakazi serikalini na mashrika ya umma.

ii) Wafanyakazi katika taasisi binafsi ambao asilimia kubwa ya mapato yake yanatokana na kufanya biashara/kushirikiana na Serikali. Katika kundi hili, wapo: Wafanyakazi wote wa vyombo vya habari.

iii) Wamiliki wa kampuni binafsi ambao mapato yao yanatokana na kufanya kazi na Serikali.

iv) Makundi yote ambayo mapato yao yanatokana na kufanyakazi/kushirikiana na Serikali.

v) Wanafunzi wote watakofaulu mtihani wa darasa la pili, la saba, vidato vya pili, nne, na sita wasome shule za Serikali.

Maelezo: Kwa kufanya hivyo, mishahara ya walimu itaboreshwa, ununuzi wa vitabu utaimarika, ujenzi wa miundombinu unaotokana na kuongezeka kwa wanafunzi kutokana na mfumo mzuri wa kutoa elimu bure kama mashimo ya vyoo, madarasa n.k. 

Hata hivyo, makundi haya ndiyo yanayopeleka watoto wao kwenye shule binafsi kwa gharama kubwa ilhali mapato yao yanagharimiwa na Watanzania maskini kupitia kodi. Hawana tofouti na baba anayewapa familia yake chakula duni ilhali yeye ‘anajichana; chips na nama choma.

Haya yakiongezwa, usawa baina ya wanajamii utaonekena; na hivyo kupunguza pengo kubwa lililopo sasa baina ya wananchi wengi wasiokuwa nacho na wachache waliokuwa na nacho.

3.6.4 Uanzishwe mfuko wa elimu kitaifa utakaochangiwa kwa utaratibu ufuatao:

i) Michango kutoka Serikali Kuu na Halmashauri zote nchini.

ii) Kwa vile wafanyakzi watakuwa wameondolewa mzigo wa kupeleka watoto wao kwenye shule ghali, kila mfanyakazi achangie asilimia tano (5%) ya maptao yake ya kila mwezi.

 iii) Ununuzi unaopitia kwa wafanybiashara wenye mashine za EFD, wachangie asilimia moja (1%) kwenye mfuko huu na makato yaende moja kwa moja kwanye mfuko huu.

 iv) Kila Halmashauri iandae utaratibu wa wananchi wake kuchangia mfuko huu. Kwa mfano, kila mwanafamilia achangie Sh 200 kwa mwezi. Hii ikiwa na maana kuwa, kama familia ina watu 10 itachangia Sh 2,000.

3.6.5 Kwa vile kutakuwa na Mfuko wa Elimu, shule binafsi ambazo zitakidhi vigezo vitakavyowekwa, zipewe ruzuku. Kwa mfano, kutekeleza ada elekezi iliyotolewa na Serikali.

3.6.6 Ili kuimarisha utoaji wa elimu na mafundisho hasa vyuo vikuu, Bodi ya Mikopo ihuishwe na kuwa Benki ya Uwezashaji wa Elimu ambako pamoja na kufanya kazi za kawaida za kibenki, itoe mikopo kwa vyuo vikuu, huku lengo likiwa ni kutoa elimu bure kutoka ngazi ya elimu ya awali hadi chuo kikuu.

Matamko haya yakitekelezwa, kwa hakika mfumo huu utakuwa endelevu nchini. Ukweli ni kwamba elimu ni ghali hivyo inatakiwa kuweka nguvu za pamoja ili wanafunzi wote wapate elimu yenye ubora sawa. Sina hakika sana na ufanisi wa Serikali kuweka ada elekezi kwa shule binafsi.

 

Suala

Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika elimu na mafunzo:  Ninapendekea kuongeza matamko yafuatayo ili kufanikisha suala hili:

3.7.5 Serikali ipitie shule zote za Serikali ili kuainisha ubora wa elimu inayotelewa kama unalenga unafanikisha malengo ya serikali kwa mtoto wa Kitanzania anapopata elimu na kama itamfanya mtoto huyo amalizapo elimu yake aweze  kusimama peke yake na Taifa kumtegemea na yeye mwenyewe kujitegemea ikiwa ni pamoja na kujiajiri.

 

3.7.6 Walimu wa shule binafsi na za Serikali walipwe mishahara na marupurupu inayofanana (ili kuondoa malalamiko ya mishahara mikubwa wanayolipwa wamiliki wa shule binafsi).

Maelezo: Matamko haya yakiongezwa nina hakika, ubia huu utafanikiwa.

 

Suala

Elimu ya sayanzi na teknolojia-uk.29

 Maelezo ya awali

Ukisoma Dira ya Taifa 2025 ibara na. 4.1(iv) inasomeka kama ifuatavyo: Mfumo wa motisha unaozingatia ubora, ubunifu, na Ustadi. Hapa ubunifu hauleti maana halisi katika matumizi ya sayansi na teknolojia. Kwa mtazamo wangu, “Ubunifu” ilitakiwa iunganishwe na Kifungu na. 4.2(iii) kinachosomeka: Ukuzaji wa Elimu ya Sayansi na Teknolijia na kusomeka kama ifuatavyo: Ukuaji  wa  Sayansi, Teknolojia na Ubunifu tofauti na hivyo Elimu ya sayansi na teknolojia inaweza isilete matokeo yanayokusudiwa kama nilivyoeleza hapo chini.

Hivyo ninapendekeza: Suala hapo juu lisomeke: Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Kwamba matunda ya sayansi na teknolojia ni uboreshaji wa bidhaa zinazotokana na ubunifu.

Sayansi, teknolojia, ugunduzi na ubunifu ni muhimu mno kwa mwanadamu  kwani  katika  historia ya dunia hakuna Taifa lolote lililowahi kuwa tajiri na lenye nguvu kama halina uwezo mkubwa na mahiri katika nyanja ya  sayansi, teknolojia, ugunduzi na ubunifu. Nchi zinazoongoza leo duniani zilifanya nini? Ziliwathamini wabunifu wao bila kujali hali au hadhi zao ilimradi walikuwa na wazo chanya ambalo lingesukuma uchumi wa nchi zao.

Kwa mfano, magari na mitambo mbalimbali ambayo nchi hizi zinajivunia, awali vilikuwa bunifu duni mno kutoka kwa wabunifu wa nchi hizi. Uongozi na mashirika ya nchi walifanya yafuatayo:

1) Walikubali bunifu hizi halafu na kuzifadhili.

2) Walijenga taasisi za kuboresha bunifu, kuzipa taasisi hizi fedha za kutosha na kuwatuza wabunifu wakati wote ubunifu wao ulipoendelea ulinufaisha Taifa. Lakini pia walihakikisha wabunifu hawa hawana msongo wa mawazo.

3) Baadhi walitoa mawazo tu. Mfano ni Sir Isaac Newton  aliyepewa heshima ya kuitwa Baba wa Sayansi japo hakugundua chochote isipokuwa kanuni zake tatu za mwendo ambazo baada ya kutumiwa na wabunifu na wataalam wengine, matokeo yake yalikuwa ni ya ajabu  kwa manufaa ya  nchi husika na dunia kama tunavyoshudia sasa. 

Lakini pia, Mgriki Pythagoras na kanuni yake maarufu katika somo la hisabati ya “Pythagoras Theorem”. Pamoja na hivyo, walizawadiwa zawadi nono.

 

 >>ITAENDELEA….

Mwandishi wa makala hii, Leonard Ndimubansi, ni msomaji mahiri wa JAMHURI. Anapatikana kupitia simu: 0713363351/0766687356; e-mail: [email protected]