“Ni wajibu wa viongozi wa Afrika kuonyesha utashi wao wa kisiasa, kwa ajili ya kuhakikisha taasisi za umajumui wa Kiafrika (pan-African) unakuwa chombo murua na kisiwe chombo cha mijadala isiyo na ukomo.”

Haya ni maneno ya aliyekuwa Rais wa Gabon, Omar Bongo, aliyefariki mwaka 2009 baada ya kuitawala nchi hiyo kwa muda mrefu.

Mugabe: Usimwamini Mzungu

“Mzungu pekee wa kumwamini ni Mzungu aliyefariki dunia.”

Haya ni maneno ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, alipokuwa katika mgogoro mzito na Waingereza mwaka 2008 kuhusu ugawaji upya wa ardhi nchini mwake. Alikuwa  akilalamika kuwa Wazungu walikuwa wamesaliti makubaliano ya Lancaster House, London, ya mwaka 1980 wakati Uingereza ilipoahidi kulipa fidia wamiliki wa mashamba ndani ya miaka 20 lakini hawakufanya hivyo.

Churchill: Maadui muhimu

“Unao maadui? Vyema. Hii inamaanisha kuna jambo umelisimamia wakati fulani katika maisha yako.”

Haya ni maneno ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill, anayechukuliwa hadi sasa kuwa ni mmoja wa viongozi waliopata kuwa na busara ya hali ya juu duniani.

Gandhi: Wakikupuuza, usiwapuuze

“Mwanzo watakupuuza, kisha watakucheka, baadaye watapambana na wewe, mwisho watakushinda.”

Haya ni maneno ya mpigania Uhuru wa India, Mahatma Gandhi, wakati akiwaeleza wapigania Uhuru kuwa wajiandae kwani harakati zao zikikubalika waliokuwa wanawapuuza wangeanza kupambana nao.

 

By Jamhuri