Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Assad amesema kwamba anaamini kwamba fedha shilingi trilioni 1.5 ambazo hazina maelezo namna zilivyotumika zitakuwa zilitumika katika maeneo mengine ya matumizi ya serikali.

Prof. Assad amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Azam Tv kuhusu fedha hizo ambazo zimezua gumzo katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari wakitaka ambapo watu wengi na wanasiasa wanataka maelezo namna fedha hizo zilivyotumika.

Wakati Mbunge Zitto Kabwe akichambua ripoti ya CAG alisema kuwa, ripoti hiyo inaonesha kwamba serikali imetumia shilingi trilioni 1.5 ambazo hazina maelezo namna zilivyotumika.

CAG akitoa ufafanuzi huo alisema kwamba, kama serikali ilitumia fedha zilizokuwa nje ya matumizi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge, ilipaswa kupeleka maombi hayo bungeni kabla ya kutumia.

Katika mitandao ya kijamii, wananchi wamekuwa wakishinikiza serikali itoe maelezo namna ilivyotumia fedha hizo kwani wana haki ya kujua.

Aidha, wananchi wengine wamelikwenda mbali zaidi wakichambua ni vitu gani ambapo fedha hiyo ingeweza kufanya, mfano kutoa huduma za afya, kujenga barabara.

 

By Jamhuri