Habari za Kimataifa

Korea Kaskazini yagoma kuharibu silaha

New York, Marekani Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Ri Yong-ho, ameonya kuwa hakuna namna ambayo nchi yake itaharibu zana za nyuklia wakati Marekani bado inaendelea kuiwekea vikwazo. Ri Yong-ho aliuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini New York, Marekani kwamba vikwazo hivyo vinapunguza imani kwa Marekani. Hivi karibuni Korea Kaskazini imerejea wito wake wa kuitaka Marekani ...

Read More »

Tetemeko laacha maafa Indonesia

Jakarta, Indonesia Watu zaidi ya 380 wamethibitishwa kufa baada ya tsunami kusababisha tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa Richter 7.5, lililopiga mji wa Jakarta mwishoni mwa wiki. Upepo mkali ulivuma kutoka Palu katika Kisiwa cha Sulewesi kwa mita tatu. Video inayoonekana kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha jinsi watu walivyokuwa wakipiga kelele huku wakikimbia kwa hofu. Baada ya mshtuko wa tetemeko ...

Read More »

Nikki Haley ajibu tuhuma za Iran, kuwa Marekani ilihusika na shambulio

Balozi wa Marekani umoja wa mataifa ameitaka Iran ijiangalie yenyewe katika shambulio la la kijeshi lililoua watu 25 siku ya Jumamosi. Balozi huyo Nikki Haley amejibu tuhuma za rais wa Iran, anayeilaumu Marekani kwa kuhusika na shambulio hilo na kusema kuwa Marekani imewagandamiza watu wake kwa muda mrefu sasa”. Makundi mawili yamedai kuhusika na shambulio hilo licha ya kutowasilisha ushahidi ...

Read More »

Mbunge wa Uganda Robert Kyagulanyi Kurejea Uganda Leo

Mbunge wa Kyandodo Mashariki mwa Uganda, Robert Kyagulanyi ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini humo ajulikanaye kama Bobi Wine anatarajia kurudi nchini Uganda leo akitokea nchini Marekani ambapo alienda kupata matibabu baada ya kupigwa na vyombo vya dola. “Nitarejea nyumbani siku ya jumatatu,licha ya kuwa bado nna hofu lakini Uganda ndio nyumbani ambapo familia yangu na watu wangu wapo.Nina wasiwasi ...

Read More »

Kimbunga Mangkhut chaua watu 30 Ufilipino chasambaa mpaka Hong Kong

Watu zaidi 30 wameuawa baada ya kimbunga Mangkhut kupiga kaskazini mwa Ufilipino. Wengi kati yao walikumbwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa. Maeneo mengi ya kisiwa cha Luzon yamejaa maji, yakiwemo mashamba ambayo huzalisha mazao makuu nchini humo ya mpunga na mahindi.

Read More »

Victiore Ingabire na Kizito Mihigo waachiliwa huru na rais Paul Kagame Rwanda

Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake kuwaachilia zaidi ya wafungwa 2000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu. Miongoni mwa wafungwa hao waliofaidika na hatua ya rais huyo ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Victoire Ingabire ambaye alikuwa katika kizuizi tangu 2010. Victoire Ingabire alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 kwa kutishia usalama wa ...

Read More »

Koffi Annan kuzikwa Ghana, Alhamisi

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, umewasili katika nchi Ghana. Mwili wake umewasili katika Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Kotoka uliopo mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa. Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi ya Taehe 13, September 2018 Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani ...

Read More »

Seneti yamaliza mahojiano, mteule wa Trump atabiriwa kuthibitishwa

Brett Kavanaugh, mteule wa Rais Donald Trump katika nafasi ya Mahakama ya Juu Marekani, Ijumaa alionekana kuwa anaelekea atapitishwa na Baraza la Seneti baada ya siku nne za mahojiano ambapo alifanikwa kujiepusha na vizingiti vikubwa pamoja na Wademokrati kujaribu kwa hasira zote kuzuia uteuzi huo. Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnel, aliulizwa na mwendesha kipindi mkonservative ...

Read More »

Baraza la Biashara Kenya laeleza madhara ya ongezeko la kodi kwenye mafuta

Kasi ya ukuaji wa uchumi wa Kenya mwaka huu huenda ikapata athari mwaka 2018 kwa kiasi kikubwa kutokana na asilimia 16 ya kodi la ongezeko la thamani (VAT) kwenye mafuta, baraza la biashara la nchi hiyo limesema Ijumaa, wakitaja bei kubwa za bidhaa na usafiri. Kodi hiyo ambayo imeanza kutumika rasmi Septemba 1, ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha ...

Read More »

Vyombo vya usalama vyawaonya wananchi wa Uganda ughaibuni

Vyombo vya usalama nchini Uganda vimewaonya wananchi wa Uganda walioko nje ya nchi ambao wanatoa matamko ya kuvunja amani, utulivu na haki binafsi za mtu yoyote hususan viongozi, watashughulikiwa ipasavyo watakapo rejea nchini. Onyo hilo limetolewa kufuatia kukamatwa kwa mtoto wa Mkuu wa Chuo cha Makerere wa zamani, ambaye polisi wanamtuhumu kwa kutumia lugha ya matusi wakati wa maandamano yaliyofanywa ...

Read More »

Obama Amshutuma Rais Trump

Aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama amemshutumu mrithi wake Donald Trump na mambo ya ‘kipuuzi yanayotoka’ katika ikulu ya Whitehouse. ”Hii sio kawaida huu ni wakati usio wa kawaida na ni wakati hatari”, Obama aliwaambia wanafunzi katika chuo kikuu cha Illinois. Alitaka kurejeshwa kwa uaminifu na heshima na sheria kufuatwa katika serikali. Rais huyo wa zamani amekuwa akifanya mambo yake ...

Read More »

Wanajeshi wa Sudan Kusini wafungwa kwa ubakaji na mauaji

Mahakama ya kijeshi imewahukumu wanajeshi 10 vifungo vya kati ya miaka saba na maisha kutokana na ghasia ambapo mwandishi wa habari aliuawa na wafanyakazi wa kutoa huduma za kibinadamu kubakwa. Mahakama imeiamrisha serikali ya Sudan Kusini kumlipa kila muathiriwa wa ubakaji dola 4,000 kama fidia. Uhalifu huo ulitokea wakati wa shambulizi lililofanywa katika hoteli ya Terrain kwenye mji mkuu Juba ...

Read More »

UN yabisha hodi Uganda

Umoja wa Mataifa (UN) umezitaka mamlaka za kisheria nchini Uganda kuitisha uchunguzi huru dhidi ya machafuko yaliyotokea nchini humo na kusababisha kukamatwa na kuteswa kwa wabunge, akiwemo nyota wa zamani wa muziki, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine. Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu wa umoja huo, Zeid Ra’ad Al Hussein, ametoa wito kwa serikali ya Rais Yoweri Museveni ...

Read More »

Askofu Aomba Radhi kwa Kumgusa Kifua Mwanamuziki

Askofu huyo aliyeongoza ibada ya mazishi ya gwiji wa muziki nchini Marekani Aretha Franklin ameomba msamaha baada ya kushutumiwa kwa kumgusa kifua mwanamuziki Ariana Grande mbele ya umati mkubwa uliohudhuria mazishi hayo. Picha zinamuonyesha Askofu Charles H Ellis wa tatu akimshika Ariana juu ya kiuno chake huku vidole vyake vikiwa vimeshikilia upande mmoja wa kifua chake. ”Sio lengo langu kumshika ...

Read More »

Bobi Wine: Aruhusiwa kuelekea Marekani kwa matibabu

Mbunge wa Uganda anayedaiwa kupigwa na wanajeshi ameruhusiwa kuondoka nchini humo , kulingana na maafisa wa polisi Hatua hiyo inajiri kufuatia madai kwamba mbunge huyo alipigwa mara kadhaa akiwa katika kizuizi cha jeshi, madai ambayo yamekataliwa na jeshi. Yeye na wanasiasa 32 wa upinzani walishtakiwa na shtaka la uhaini wiki iliopita kufautia madai ya kuupiga mawe msafara wa rais Yoweri ...

Read More »

Watanzania 27 wasio na vibali wakamatwa Mombasa nchini Kenya

Watanzania 27 wamekamatwa mjini Mombasa Kenya baada ya kuingia nchini humo bila vibali maalum. Mamlaka ya usalama huko Mombasa inaendelea na mipango ya kuwarejesha nchini kwao. Baadhi ya watu hao wameshikiliwa na polisi katika kituo cha Likoni wakati wakisubiri kurejeshwa nyumbani. Kamanda wa polisi wa Mombasa Johston Ipara ameeleza kwamba Watanzania hao ni miongoni mwa wahamiaji wengine kutoka Congo, Somalia, ...

Read More »

Bobi Wine kufikishwa mahakama ya kijeshi leo.

Mbunge ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki nchini Uganda Robert Kyagulanyi jina maarufu Bobi Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda. Taarifa hiyo imewashtua mawakili wake ambao awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala. Wakati huo huo Mtandao wa haki za binadamu za wanahabari nchini Uganda umetoa saa 48 ...

Read More »

Maandamano yazuka Kampala kupinga kukamatwa mbunge Bobi Wine

Vikosi vya usalama nchini Uganda wamewakamata watu 10 waliojihusisha na maandamano ya kupinga kukamatwa kwa Mbunge wa upinzani, Bobi Wine ambaye alikamatwa na kushitakiwa kwenye Mahakama ya Kijeshi wiki iliyopita. Shughuli za Biashara zimesimama katika Jiji la Kampala, leo Mchana kutokana na makabiliano makubwa kati ya Vikosi vya usalama dhidi ya Wananchi ambao waliojitokeza kwenye maandamano hayo. Wandamanaji wamechoma moto ...

Read More »

Familia za Korea Kaskazini na Kusini zilizotenganishwa na vita zakutana kwa mara ya kwanza

Kundi la watu wazee kutoka Korea Kusini kwa sasa wako nchini Korea Kaskazini kukutana na jamaa zao wenye hawajawaona tangu vimalizike vita vya mwaka 1950-1953. Vita hivyo vilisababisha rasi ya Korea kutengana na watu waliokuwa wanaishi upande wa Kaskazini wasikuwe na uwezo wa kuondoka. Korea hizo mbili ambazo bado ziko kwenye mzozo wa vita, zilikuwa zimepanga shughuli ya kuwakutanisha watu ...

Read More »

Basi la abiria lateketea kwa moto Kigoma

Basi la Kampuni ya Saratoga lenye namba za usajili T476 ADG lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda Sumbawanga limeteketea kwa moto eneo la Kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma. Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Ottieno limesema kuwa bado linachunguza chanzo cha moto huo. Kwa mujibu wa Kamanda huyo, abiria wote wametoka salama na baadhi ...

Read More »

Rais wa Uganda Museveni anakanusha kwamba Bobi Wine amejeruhiwa

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekanusha kwamba mbunge wa upinzani Bobi Wine amejeruhiwa. Katika taarifa yake ya kwanza kuhusu afya ya mbunge huyo aliyekamatwa na vikosi vya usalama nchini, Museveni amevishutumu vyombo vya habari kwa kile alichokitaja ni kueneza habari zisizo za kweli kuhusu suala hilo. Kulingana na ripoti mbalimbali za vyombo vya habari mbunge huyo ambaye pia ni msanii, ...

Read More »

Tutaendelea Kumkumbuka Kofia Annan

Jana August 18, 2018 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amefariki jana Agosti 18 nchini Uswisi akiwa na umri wa mika 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Inaelezwa kuwa Annan ambae alikuwa ni Raia wa Ghana anatajwa kuwa Mtu wa kwanza mweusi kutoka Afrika kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoka mwaka 1997 mpaka mwaka ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons