Uchumi

RC WANGABO: Wenye Madeni Lazima Wakatiwe Maji

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo ameiagiza Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA) kuwakatia maji wateja wenye madeni sugu ili waweze kulipa madeni yao wanayodaiwa na taasisi mbalimbali za serikali nchini.   Amesema kuwa uendeshaji wa Mamlaka hiyo utaendelea kuwa mgumu endapo wataendelea kuwafumbia macho wateja wanaowadai na kushauri kuanza kuangalia namna ya kutumia kadi ...

Read More »

Mapya yamfika Muhongo

Mambo hubadilika ghafla. Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, anatarajiwa kuhojiwa na vyombo vya usalama leo kutokana na sakata la mchanga wenye madini. Habari za uhakika zilizolifikia JAMHURI zimethibitisha kuwa Prof. Muhongo atahojiwa kuhusiana na ripoti ya uchunguzi  wa mchanga wa madini, ambao umekuwa ukisafirishwa nje ya nchi kwa makontena tangu mwaka 1998. Muhongo anahojiwa kutokana kushindwa ...

Read More »

Ulaji wa kutisha bungeni

Mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Bunge, ya kumlipa kila mbunge mafao ya Sh milioni 238 baada ya Bunge kuvunjwa mwezi ujao, yanazidi kuichanganya Serikali. Duru za uchunguzi zinaonyesha kuwa tayari Serikali inakabiliwa na ukata mkubwa, kiasi cha kusuasua kuwalipa wabunge mishahara yao ya kila mwezi. Mishahara ya mwezi Mei ililipwa mwanzoni mwa mwezi huu. Mzigo wa malipo hayo mapya ...

Read More »

AGPAHI yamwaga misaada Shinyanga

Shirika la AGPAHI, linalojihusisha na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI, limezindua majengo mawili kwa ajili ya Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na vimelea hivyo.   Shirika hilo linalofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimarekani (CDC) nchini Tanzania, limezindua majengo hayo kwenye Zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama, na Kituo cha Afya ...

Read More »

GST yaongeza thamani madini ya nikeli

Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kupitia maabara yake ya utafiti wa madini, imefanikiwa kuongeza thamani ya madini ya nikeli (Ni) kutoka katika mbale za Milima ya Mahanza-Haneti mkoani Dodoma.   Akizungumza na MEM Bulletin, Mhandisi Priscus Kaspana, mmoja wa wanajopo la watafiti kutoka GST, anasema kuwa utafiti huo ulianza Machi 2015, na tayari sampuli nne zimefanyiwa utafiti wa uongezaji thamani ...

Read More »

Ripoti yabaini madudu zaidi TRL

Ripoti ya awali kuhusu uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa mabovu uliofanywa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), imebaini kuwa menejimenti ya kampuni hiyo haikuwa makini kushughulikia maombi ya kuongezewa muda, yaliyowasilishwa na Kampuni ya Hindusthan Engineering and Industries Limited ya nchini India.   Uchunguzi umebaini kuwa mkataba wa zabuni namba PA/113/2012-13/ME/G/OE/014 ya ununuzi wa mabehewa 274 ya mizigo, Kampuni ...

Read More »

‘Serikali imekurupuka, imeumbuka’

Serikali imeingia doa. Migomo wafanyabiashara na madereva wanaoendesha mabasi ya abiria, imetikisa nchi kiasi cha kufanya wadau kadhaa kueleza kuwa nchi imekosa sifa za uongozi. Tukio la kwanza, ambalo limekuwa likijirudia linahusu wafanyabiashara ambao mara kwa mara wamekuwa wakigoma kwa kufunga maduka kwa shinikizo la kuachiwa Mwenyekiti wao, Johnson Minja. Tukio la pili ni la madereva, ambao Ijumaa iliyopita walitekeleza ...

Read More »

Wizara kuwapatia maji Sengerema

Mhandisi wa Maji, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Wawa Nyonyoli, ametangaza kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wakazi wa mji huo watapata maji safi na salama ifikapo Juni, mwaka huu.  Akizungumza na mwandishi wa JAMHURI mjini hapa, Mhandisi Nyonyoli anasema kwamba mradi huo unaratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).   Anasema kwamba ...

Read More »

Tanroads yafanya kweli

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umenunua mtambo wa kisasa wa kukagua madaraja marefu yenye maji na kurahisisha shughuli hiyo, tofauti na njia iliyokuwa ikitumika awali ya kutumia kamba iliyohatarisha maisha wataalamu. Mtambo huo wa kisasa (Bridge Inspection Vehicle) ambao umeanza kutumika Tanzania, kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, umegharimu Sh. bilioni 1.2 na utatumika kupima madaraja mbalimbali nchini. Mhandisi ...

Read More »

Sababu za kufeli hizi hapa

  Umbali mrefu kati ya shule za sekondari za kata na makazi ya wanafunzi unachangia kwa kiasi kikubwa ‘anguko’ la wanafunzi katika matokeo ya mwisho ya wahitimu wa kidato cha nne kila mwaka.  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda wa miezi mitano umebaini kuwa ufaulu hafifu wa wanafunzi hao husababishwa na umbali mrefu uliopo kati ya shule na makazi ...

Read More »

Walarushwa hawa hapa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imetangaza hadharani washitakiwa wote waliopatikana na hatia katika kesi zinazohusu rushwa.  Taarifa ya ambayo gazeti hili imeipata inasema kutajwa kwa washitakiwa hao ni utaratibu mpya unaoanza kutumika mwezi huu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN). Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani, analithibitishia gazeti ...

Read More »

Nauli za daladala kushuka Machi 18

Nauli za daladala nchini zinatarajia kushuka mwishoni mwa mwezi huu kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta nchini na duniani kwa ujumla.   Mwenyekiti  wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DRCOBOA), Sabri Mabrouk, ameiambia JAMHURI kuwa wamiliki wa daladala watakumbwa na “msiba mkubwa hivi karibuni” kutokana na msimamo wa Serikali ambayo inatarajia kushusha nauli kutokana ...

Read More »

Bandari Dar inakufa

*Mkurugenzi Mkuu Kipande aingiza ukabila, udini, majungu

*Wafanyakazi watatu bandarini wafariki kutokana na vitisho

*CCTV hazifanyi kazi tangu 2011, wachonga dola mil. 6.5

*Mnikulu Gurumo, Mtawa wampa kiburi, wachafua jina la JK

*Amdanganya Dk. Mwakyembe, amtukana Balozi wa Japan

Kuna kila dalili kuwa Bandari ya Dar es Salaam inakufa kutokana na uongozi mbovu uliojiingiza katika majungu, udini, ukabila na majivuno yasiyo na tija. Wafanyakazi katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamepoteza morali wa kufanya kazi kutokana na vitisho na matusi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Madeni Juma Kipande.

Hadi habari hii ya kiuchunguzi inachapishwa wafanayakazi watatu; Peter Gwamaka Kitangalala, Dotto Mbega na mwingine aliyefahamika kwa jina la Lyochi wamefariki dunia katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na shinikizo la damu lililozaa kiharusi baada ya vitisho vya Kipande.

Katika hali ya kuwavuruga wafanyakazi wa bandari, Katangalala alihamishiwa Mwanza na baada ya miezi miwili akahamishwa tena kwenda Lindi, huku akipewa vitisho kuwa muda wowote ajiandae kufukuzwa kazi. Kutokana na hofu, alipata kiharusi (stroke) akafa. Mbega kwa upande wake yeye alikuwa makao makuu Dar es Salaam, lakini kutokana na vitisho vya kila siku vya Kipande na wasaidizi wake, naye akapata kiharusi mwezi mmoja uliopita akafariki dunia.

Jumapili ya Machi 30, mfanyakazi mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Lyochi huku wengine wakisema ni Oluwochi mwenye asili ya Wajaruo, aliyehamishiwa bandari ya Kasanga, Sumbawanga naye aliaga dunia kwa ugonjwa huo huo wa kiharusi kutokana na mashinikizo ya Kipande.

“Uhalisia hali inatisha. Kipande anajinadi kuwa atamfukuza kila mtu, na kweli anafukuza anaajiri watu wa dini yake. Kuna kabila la Wahaya kutoka Kanda ya Ziwa, hilo utadhani waliwahi kushikana nalo ugoni. Mhaya yeyote aliyemkuta kazini ameapa kumg’oa. Amehamisha [Hassan M.] Kyomile kwa sababu ya kabila lake na kwamba aliomba kazi ya Ukurugenzi Mkuu,” kilisema chanzo chetu.

Kyomile amehamishwa Machi mwaka huu, kutoka makao makuu alikokuwa Mkurugenzi wa Ununuzi na kwenda kuwa Meneja wa Bandari Tanga.

Read More »

Mwalimu amtia mimba mwanafunzi

Mwalimu Nelson Bashulula anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya kutwa ya Rubale iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera, anatuhumiwa kwa kosa la kumtia mimba mwanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo (jina linahifadhiwa).

Read More »

Maswi: Kila Mtanzania atapata umeme

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imesema umeme ni huduma ya lazima kwa Watanzania na itafanya kila liwalo kuhakikisha kila Mtanzania anapata umeme. Msimamo wa Serikali umetolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, wakati akizungumza katika kipindi cha Tuambie kupitia runinga ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wiki iliyopita.

Read More »

Muhongo akagua ujenzi bomba la gesi

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameeleza kuridhishwa kwake na kasi ya utandazaji na uunganishwaji wa mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

Read More »

Matapeli wakubwa Tanzania hadharani

RIPOTI MAALUM

*Watumia madini kutapeli Wazungu hadi bilioni 160/-, watamba

*Mwanza, Dar, DRC, Zambia, Papa Msofe, Aurora waongoza ‘jeshi’

*BoT, NBC, Exim Bank, Polisi, Mahakama, Uhamiaji nao watumika.

 

Baada ya sifa ya Tanzania kuingia doa kutokana na watu wengi maarufu kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa matajiri wengi nchini wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kutupwa kwa Wazungu kupitia ahadi hewa za kuwauzia madini.

Read More »

Mtendaji mkuu Osha alalamikiwa Tughe

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, amelalamikiwa mbele ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), kuwa anawaongoza kimabavu wafanyakazi wa taasisi hiyo ya Serikali.

Read More »

UNESCO, WHC wakubali barabara NCAA-SENAPA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kituo cha Urithi wa Dunia (WHC) wameikubalia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ifanye upembuzi yakinifu wa barabara ya Lodoare-Serengeti.

Read More »

Wanaume watelekeza watoto walemavu Arumeru

*Wanawake wasukumiwa mzigo

Tatizo la wanaume kuwatelekeza watoto wao wenye ulemavu, limetajwa kukithiri katika Kijiji cha Ambureni, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.

Read More »

Utajiri wa Obama Sh bilioni 32

Dhana kwamba wanasiasa wanapaswa kuwa watu maskini huenda imepitwa na wakati. Rais wa Marekani, Barack Obama yeye na familia yake wanamiliki utajiri wa dola 19,225,070 sawa na Sh 31,529,114,800.

Read More »

Ujio wa Obama wabadili mfumo Dar

Ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, hapa Tanzania imebadili mfumo mzima wa matumizi ya barabara na shughuli mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons