[caption id="attachment_73" align="alignleft" width="314"]
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki[/caption]*Kiini macho chaibuka vitalu vya WMA
*Vyatangazwa Kagasheki akiapa Ikulu
*Ni kukamilisha ratiba, matajiri wavinasa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, anakabiliwa na mtihani wa kwanza ndani ya wizara hiyo, baada ya kuibuka kwa kashfa mpya katika ugawaji vitalu 13 vya uwindaji vinavyomilikiwa na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs).
Vitalu hivyo ni tofauti na vile vilivyosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Ezekiel Maige. Habari za uhakika kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na katika WMA, zinaonyesha kuwa kutangazwa kwa vitalu hivyo kumefanywa haraka haraka siku Kagasheni na mawaziri wenzake walipokuwa Ikulu wakiapishwa.