Nyundo ya Wiki

Polisi waomba Kitwanga, IGP wawanusuru

Baadhi ya askari polisi katika maeneo mbalimbali wamewaomba Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu kuingilia kati kuwanusuru na unyanyasaji wanaofanyiwa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCDs), wanaowahamisha vitengo kwa uonevu. Wakati wakieleza kuwa IGP Mangu ametoa agizo askari wapanguliwe kwa baadhi kutolewa Trafiki na Upelelezi kwenda General Duties, ...

Read More »

Waziri aunda mchongo kabla ya kuachia ofisi

Mgogoro mkubwa umeibuka ukiwahusisha wafanyabiashara ya uwindaji wa kitalii na Serikali. Chanzo cha mtafaruku huo ni uamuzi wa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, siku chache kabla kuachia ofisi, kufuta Kanuni za Uwindaji wa Kitalii za mwaka 2010 na kutunga Kanuni mpya. Kanuni hizo mpya ambazo hazikuwashirikisha wadau zimeshaanza kutumika kupitia Tangazo la Serikali Na. 414. Nyalandu alihakikisha ...

Read More »

Lowassa, Maalim Seif waitesa CCM

Wagombea wa urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Maalim Seif Sharif Hamad kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wameikaba koo Serikali. Licha ya vikao kadhaa na viongozi wa Serikali, wote kwa pamoja hawakubaliani na matakwa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachofurahia kurudia Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar baada ...

Read More »

Sitta amesahau nini bungeni?

Mwanasiasa wa siku nyingi, Samuel Sitta, ametangaza nia ya kuwania kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuna sentesi maarufu ya: “ni haki yake ya kikatiba.” Sawa, ni haki yake, lakini hata sisi wananchi tuna haki ya kutoa maoni yetu. Mzee Sitta (73) alizaliwa Desemba 18, 1942. Amekuwa Mbunge kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1995. Ameshakuwa ...

Read More »

Mbowe: Hatuwezi kukata tamaa

Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu umeiweka nchi katika historia nzuri na mbaya, kutokana na kuimarika kwa vyama vya siasa vya ushindani huku dosari nyingi zilizojitokeza. Idadi kubwa ya wananchi waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura walijitokeza katika kampeni za vyama vya siasa, kuwasikiliza wagombea waliokuwa wakijinadi na kushiriki katika Uchaguzi Mkuu. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amefanikiwa ...

Read More »

Lowassa hajanihonga – Mramba

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema hajahongwa kiasi chochote cha fedha na wadau mbalimbali akiwamo Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, kama inavyodaiwa. Taarifa zilizopo zinadai kwamba Mramba amehongwa Sh. bilioni 4 na Lowassa ambaye kwenye harakati za kuisaka Ikulu anaungwa mkono na vyama vinavyopigania Katiba yenye maoni ya wananchi (Ukawa). Taarifa hizo zilithibitishwa ...

Read More »

Ndani ya Dk. Magufuli namuona Mwl Nyerere

Nimepata muda wa kukaa na Dk. John Magufuli, kwa nyakati mbalimbali tangu akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi hadi sasa anapowania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwanasiasa huyu anayepewa nafasi kubwa ya kushinda kiti cha urais, ni mfuasi mzuri sana wa fikra za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kwa yeyote anayekaa na Dk. Magufuli, ni nadra mno ...

Read More »

Mabadiliko Polisi, kampeni zamngo’a RPC Konyo Geita

Wakati kampeni za urais, ubunge na udiwani zikiendelea nchini, joto la uchaguzi limepamba moto kiasi cha kumponza Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Geita, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Joseph Konyo. Taarifa za uhakika kutoka Jeshi la polisi Dar es Salaam, zinasema kuwa ACP Konyo ameondolewa eneo hilo la kazi na kurejeshwa Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini, atakakopangiwa majukumu ...

Read More »

SAMIA: Tutachapa kazi kama mchwa

Kama kuna mambo yatakayobaki kwenye historia nchi baada ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, ni kuwapa nafasi wanawake katika vyombo vya uamuzi. Mbali ya kuteua wakuu wengi wa wilaya, mikoa, majaji ni Rais Kikwete aliyeonekana kuwa na kiu akitaka moja ya nguzo za dola kuongozwa na mwanamke. Kupitia taratibu mwafaka, Anne Makinda-Mbunge wa Njombe Kusini akateuliwa na chama na kuchaguliwa ...

Read More »

Waathirika Operesheni Tokomeza waibuka

Kiongozi wa Kamati ya Wafugaji kutoka Kijiji cha Lumbe, Kata ya Ukumbisiganga, Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, amepiga kambi jijini Dar es Salaam akililia fidia ya ng’ombe 2,537 waliopotea kwenye ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’ iliyofanyika Oktoba 2013. Wakati wenzake wakirudi nyumbani, kiongozi huyo, Mashili Shija, anasema anapambana kutaka kuonana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kupata majibu ya hatima ya mali ...

Read More »

Dimbwi halisababishi mafuriko

Mafuriko  ni wingi wa maji uliopitiliza, wingi huo wa maji hutokana na nguvu za asili. Hakuna mwanadamu awezaye kuyatengeneza mafuriko kama ilivyo vigumu kwa kuyazuia, hakuna awezaye kuyazuia mafuriko. Hiyo ni nguvu ya asili.  Pamoja na ujanja wote wa binadamu bado hajaweza kuizuia nguvu ya asili.  Bwawa la maji hata liwe na ukubwa wa aina gani, kama bwawa lenyewe ni ...

Read More »

Wampinga JK kwa Magufuli

Rais Jakaya Kikwete ameibua hisia za baadhi ya akina mama wanaopinga hoja yake inayosema kwamba mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli ni “Chaguo la Mungu”. Akinamama hao waliokuwa wakishiriki kongamano la maombi na amani nchini wameeleza kuwa uteuzi wa Dk. Magufuli ndani ya CCM uligubikwa na migongano ya rushwa na ...

Read More »

Sumbawanga yanuka ufisadi

Vigogo wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wamedaiwa kutengeneza vitabu bandia vya kukusanyia mapato ya ushuru na leseni za  uvuvi kwa wafanyabiashara wa samaki katika Ziwa Rukwa, JAMHURI inaripoti.  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba vitabu hivyo vimetengenezwa na baadhi ya wakuu wa idara ndani ya manispaa hiyo, kwa lengo kujiingizia mapato yanayokadiriwa kufikia zaidi ya Sh. milioni 100 ambazo ...

Read More »

Mzungu mchochezi anaswa Loliondo

Raia wa Sweden, Susanna Nordlund, anayetambuliwa kama mmoja wa wachochezi wakuu wa migogoro katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha, amekamatwa na kufukuzwa nchini. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Ngorongoro, Hashim Shaibu, ndiye aliyeongoza Kamati hiyo kwenda kumkamata. Sussana alikamatwa saa 2 usiku katika hoteli maarufu ya Onesmo iliyopo Wasso, akiwa anakula ...

Read More »

Manispaa Kinondoni ‘yauza’ barabara

Serikali Kuu na Manispaa ya Kinondoni wameruhusu ujenzi wa Shule ya Saint Florence Academy iliyopo Mikocheni “B”, Dar es Salaam juu ya barabara. Hatua hiyo, licha ya kuwa imevunja sheria za Mipango Miji, imekuwa kero na hatari kwa usalama wa wanafunzi na majirani wa kiwanja hicho namba 622. Pia imebainika kuwa mmiliki wa shule hiyo pamoja na familia yake, wanaishi ...

Read More »

Wazee ‘wamaliza kazi’ CCM

Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), limeshatoa mapendekezo ya awali ya kumsaidia Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ili kumpata mgombea urais atakayekiwakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu. Baraza hilo linaundwa na wenyeviti na makamu wenyeviti wastaafu. Wajumbe wake ni marais wastaafu – Ali Hassan Mwinyi (Mwenyekiti), Benjamin Mkapa, Dk. Salmin Amour, ...

Read More »

Yanayoendelea Afrika Kusini ni mwendelezo wa ubeberu

Hisia tupu hazitusaidii kuzikabili changamoto zenye uhalisia mwingi. Kiendeleacho Afrika Kusini ni matokeo ya muda mrefu wa kupandwa kwa saratani ya ubaguzi wa kijamii, kisiasa na kiuchumi.  Haiyumkiniki ni kile kitarajiwacho baada ya jamii na tawala kujisahau, wakatokea kudunisha baadhi ya watu na kusimika unyonyaji, dhuluma iliyotopea na kusakafia ubeberu kinyume cha thamani kuu ya utu.  Ninaamini bado wengi wa ...

Read More »

RC K’njaro amilikisha marehemu kiwanja

Ndugu zangu wanahabari, Januari 30 mwaka huu, niliwaiteni na kuwaeleza kwa kirefu kuhusu mgogoro wa kiwanja kilichokuwa na hati namba 10660 ambacho ndipo zilipo Ofisi za Kata ya Mawenzi ambacho zamani kilikuwa kikimilikiwa na The Registered Trustees of Mawenzi Sports Club kabla ya kutwaliwa na Serikali mwaka 2002. Lakini kama mtakavyokumbuka, niliwaeleza namna Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ...

Read More »

Ugaidi Tanzania

Serikali imetakiwa iwe makini kuhakikisha inavitumia vyombo vyake vya ulinzi na usalama na wananchi kukabiliana na tishio la makundi ya kigaidi, hasa al-Shaabab kutoka Somalia. Mbunge wa Kigoma Kusini – NCCR-Mageuzi, David Kafulila ameliambia JAMHURI kwamba Tanzania inapaswa kuwa makini. Anasema suala la ugaidi linalozungumzwa kila mahali nchini linaweza kufanyika kutokana na magaidi kutekeleza uhalifu huo bila kujulikana kirahisi. Kwa ...

Read More »

‘Serikali imekurupuka, imeumbuka’

Serikali imeingia doa. Migomo wafanyabiashara na madereva wanaoendesha mabasi ya abiria, imetikisa nchi kiasi cha kufanya wadau kadhaa kueleza kuwa nchi imekosa sifa za uongozi. Tukio la kwanza, ambalo limekuwa likijirudia linahusu wafanyabiashara ambao mara kwa mara wamekuwa wakigoma kwa kufunga maduka kwa shinikizo la kuachiwa Mwenyekiti wao, Johnson Minja. Tukio la pili ni la madereva, ambao Ijumaa iliyopita walitekeleza ...

Read More »

Mahakama ya Kadhi fupa gumu bungeni

Kabla ya kuwasilishwa bungeni Aprili mosi, mwaka huu muswada wa Mahakama ya Kadhi, ulipata ugumu wa aina yake kwenye semina ya wa wabunge iliyolenga kuwaongezea ufahamu juu ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.  Hata hivyo, kile kilichotokea kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma, ilitosha mamlaka husika kuondoa muswaada bungeni. Semina hiyo iliandaliwa na Wizara ya Katiba na ...

Read More »

Sababu za kufeli hizi hapa

  Umbali mrefu kati ya shule za sekondari za kata na makazi ya wanafunzi unachangia kwa kiasi kikubwa ‘anguko’ la wanafunzi katika matokeo ya mwisho ya wahitimu wa kidato cha nne kila mwaka.  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda wa miezi mitano umebaini kuwa ufaulu hafifu wa wanafunzi hao husababishwa na umbali mrefu uliopo kati ya shule na makazi ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons