Michezo

Seki Chambua amtia ndimu Simon Msuva

Wakati mshambuliaji chipukizi wa yanga mwenye kasi, Simon Msuva, akimaliza majaribio yake nchini Afrika Kusini, wadau mbalimbali wa soka wamempongeza kwa kuthubutu. Ingawa uongozi wa Klabu ya Yanga ulisema kuwa unakusudia kumuadhibu mchezaji huyo na klabu aliyokwenda kufanya majaribio, lakini baadhi ya wadau wanasema amechukua uamuzi sahihi. Baadhi ya wadau wanauunga mkono uongozi wa Yanga, uliosema kuwa utamuadhibu Msuva kwa ...

Read More »

Simba yaonywa usajili

Wakati tetesi za usajili zikizidi kushika kasi nchini katika klabu mbalimbali, uongozi wa Wekundu wa Msimbazi  Simba Sports Club ya Dar es Salaam, umeonywa kuwa makini katika jambo hilo. Simba inayohaha kushika angalau nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ili icheze Kombe la Shirikisho (CAF) mwakani, kuna taarifa kuwa ina ratiba ya kujaza mapengo. Taarifa hizo zimewafikia ...

Read More »

Cannavaro afufua matumaini, Yanga ikiifuata Etoile

Matumani ya kufanya maajabu ugenini kwa upande wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, yamefufuka baada ya taarifa za kitabibu kusema Nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, atakuwa fiti kuwakabili Waarabu. Yanga wanaotarajiwa kuondoka nchini kesho Jumatano kwenda Tunisia kurudiana na Etoile du Sahel katika mechi ya Kombe la Shirikisho, ilimkosa mchezaji huyo katika kipindi cha pili cha ...

Read More »

Weusi wa Balotelli watikisa

Mshambuliaji wa Liverpool, Mtaliano Mario Balotelli, ndiye mchezaji aliyebaguliwa zaidi katika Ligi Kuu ya England, imefahamika.  Taarifa zinasema kwamba mchezaji huyo hupokea ujumbe wa aina mbalimbali katika mitandao ya Twitter, Facebook, Instagram na WhatsApp ambako jumla yake ni 8,000 kwa siku.  Lakini wakati akipokea mjumbe huo, asilimia 50 yake umekuwa ni wa kibaguzi kiasi cha kumfanya nyota huyo wa zamani ...

Read More »

Morris, Kipre warudi Azam

Mara baada ya kuwatosa kwa muda wachezaji wake, Kipre Tchetche na Aggrey Morris, timu ya soka ya Azam FC imewarejesha haraka ili kujiweka sawa kwa ajili ya kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu Bara.  Wachezaji hao walifungiwa kucheza mechi nne baada ya kubainika kufanya kosa la kuondoka kambini bila kuaga, lakini kabla ya adhabu hiyo kufika mwisho wamerudishwa kundini.  Katika mechi ...

Read More »

Salum Abdallah aliuza nyumba kununua vyombo vya muziki

Mji wa Morogoro ni miongoni mwa miji iliyokuwa maarufu kwa michezo na burudani katika miaka ya 1950, 1960 na ya 1970.   Watu wengi walitoka Dar es Salaam na kwenda kufanya starehe za kumaliza wiki mjini humo. Hali ya hewa na kuwapo kwa bendi mbili maarufu zilizokuwa na uwezo mkubwa, ilifanya wafanyakazi wengi watamani kupangwa kufanya kazi mjini Morogoro.   ...

Read More »

Snake Junior ndio kama mlivyosikia

Wakati mashabiki wa ngumi wakisubiri pambano la kukata na shoka kati ya mabondia mahiri duniani, Manny ‘Pacman’ Pacquiao na Floyd Mayweather, mambo yamekuwa mabaya kwa bondia kinda wa Tanzania, Mohammed ‘Snake Jr’ Matumla. Snake Junior-mtoto wa bondia mahiri wa zamani wa Tanzania, Rashid ‘Snakeman’ Matumla, alikuwa na ahadi ya kucheza pambano la utangulizi katika uliongo ulipangwa kutumiwa na akina Pacman ...

Read More »

Aveva apewa somo zito Simba

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba inashika nafasi ya tatu mbele ya kinara Yanga na Azam, lakini taarifa za ndani ya klabu hiyo, zinasema kwamba haikustahili kuwa hapo hadi sasa. Mmoja wa viongozi wa timu hiyo anasema kwamba itakuwa ni vigumu kwa Simba kutwaa taji la Ligi Kuu Bara kwani kuna tatizo kubwa la uongozi kushindwa kufuatilia mtiririko wa ...

Read More »

Mtego mkali ulitumika kuinasa Sosolis

  Bendi ya Trio Madjes 'Sosoliso' ilikuwa imesheheni vijana na kuweza kulitikisa jiji la Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika muziki. Chanzo cha kuanzishwa kwa bendi hiyo kunaelezwa kuwa kulitokana na kuporomoka kwa Bendi ya Orchestra Veve baada ya wanamuziki wake wengi kuiacha bendi hiyo. Mwanamuziki Kiamungwana Wazolambongo Mateta Verckys, alikuwa kiongozi wa bendi hiyo ya Orchestra Veve ...

Read More »

Takururu yamulika rushwa Ligi Kuu

Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) imepanga kuzikomalia timu za Yanga, Azam na Simba zenye nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) hili kudhibiti upangaji matokeo katika mechi za mwisho wa msimu huu.  Timu hizo ambazo zinashika nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo zimekuwa walengwa wakubwa katika kudhibiti kupanga matokeo kutokana ...

Read More »

Pluijm anogewa michuano ya kimataifa

Kocha wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Mholanzi Hans van der Pluijm, amewaambia wachezaji kwamba kama wanataka kuendelea kupanda ndege na kucheza mechi za kimataifa, basi hawana budi kutwaa ubingwa wa Bara. Kocha huyo anasema anaamini wachezaji wa Yanga wana uwezo mkubwa kufanya vizuri kama watakubali kujituma na kupambana kwa hali na mali kufikia mafanikio ya zaidi ya ...

Read More »

Walcot adai anaiva na Wenger

  Mshambuliaji wa Arsenal 'the Gunners', Theo Walcot, anasema kuwa hajakosana na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Arsene Wenger, na kuongeza kwamba hajaanza mazungumzo ya mkataba mpya na klabu hiyo.   Mkataba wa Walcot unakamilika mwaka 2016 na Wenger amesema kuwa anatarajia kuwa na muda mrefu wa makubaliano na mchezaji huyo kuhusishwa kuwa atamtosa na kumsajili Marco Reus wa Borussia ...

Read More »

Kopu amshtua Casillas, Ngassa abaniwa Yanga

  Kocha Mkuu wa Simba ya Dar es Salaam, Goran Kopunovic, amekaa na kipa wa timu hiyo, Hussein Sharrif 'Casillas', na kumwambia hana budi kukaza msuli ili aanze kukaa golini kulinda lango kama zamani.   “Ndiyo, nimekaa naye na kumweleza Casillas ajitahidi,” anasema Kopunovic alipozungumza na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa wiki iliyopita. Amesema kwamba kipa huyo ana nafasi ...

Read More »

Okwi amtaja Marco Reus

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, amemtaja Marco Reus wa Borussia Dortmund kuwa ndiye anayefanya apige mabao ya kiufundi dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar, na kusababisha mabao hayo kuwa gumzo.   Akizungumza na JAMHURI hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa njia ya simu, Okwi anasema amejifunza aina hiyo ya ufungaji kutoka kwa Reus, kiungo mshambuliaji wa Ujerumani.   “Huyo ...

Read More »

Maskini England, haina chake 2015

Wakati mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Uropa yakiingia hatua ya robo fainali, hali imekuwa mbaya kwa England kwa mwaka huu, baada ya timu zake zote kuondolewa kwenye michuano hiyo mikubwa yenye mvuto wa aina yake Ulaya.   Everton iliyosalia hadi Alhamisi wiki iliyopita kwenye michuano ya Uropa, nayo ilikutana na balaa lililowapata Chelsea, Manchester City, Arsenal zilizokuwa zinashiriki ...

Read More »

Phiri aifuta Simba ubingwa wa Bara

Kocha wa zamani wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, amewashauri Simba kuacha kuwaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na kuwataka kupigania angalau nafasi ya pili katika msimamo.   Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa makala hii, Phiri, aliyetimuliwa Simba katikati ya msimu huu, anasema Simba ni timu bora, lakini wana changamoto kubwa.   Anasema kuwa kama wanang'ang'ania kutaka ...

Read More »

Mourinho apandisha hasira Chelsea

Licha ya kubezwa, hasa kwa kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Chelsea imeamua kuhamishia hasira zake kwenye Ligi Kuu England (EPL) ambako inaongoza kwenye msimamo.   Kocha Mkuu wa timu hiyo, Jose Mourinho, amesema katu sasa hawatang'oka katika nafasi hiyo ya kinara katika msimamo na malengo sasa ni kushinda taji.   Chelsea maarufu kama The Blues wametupwa nje katika michuano ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons