Michezo

Tambo zaanza kuelekea Afcon

Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Uganda, Sebastien Desabre, amesema timu ya taifa ya soka ya Zimbabwe ina nafasi finyu katika kundi ‘A’ kwenye michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baadaye mwezi Juni, mwaka huu. Uganda itakabiliana na mwenyeji wa michuano hiyo, Misri, DR Congo na Zimbabwe katika kundi ‘A’. Kocha huyo kwa upande ...

Read More »

Simba SC ni ‘half time’

Dakika 90 kati ya 180 za mchezo wa robo fainali ya Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika baina ya Simba SC na TP Mazembe zimekamilika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa miamba hao kutoka suluhu. Klabu ya Simba imekuwa ikiheshimika huko nje kwa kutumia vema uwanja wake wa nyumbani, hasa ikikumbukwa kwamba ilipata matokeo chanya dhidi ya ...

Read More »

Yanga kutetema mbele ya Lipuli?

Timu ya Yanga imeendelea kugawa dozi kwenye Kombe la FA, baada ya kufuzu kuingia katika hatua ya nusu fainali, baada ya kuwatupa nje ya michuano hiyo timu ya Alliance kwa jumla ya penalti 4-3 katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1. Katika hatua hiyo ya robo fainali, mchezo huo wa ...

Read More »

Babu Miura bado anakiwasha

Ng’ombe hazeeki maini, Waswahili ndivyo wanavyosema. Kazuyoshi Miura, ndiye anayetajwa kuwa mchezaji wa soka mwenye umri mkubwa zaidi duniani. Inaelezwa kuwa licha ya kuwa na umri wa miaka 52, bado anasakata kabumbu katika timu ya Yokohama inayoshiriki Ligi Kuu nchini Japan. Miura pia anafahamika kwa jina la ‘King Kazu’, kutokana na kucheza miondoko ya ‘kazu’ pindi anapofunga magoli. Miura ni ...

Read More »

‘Bravo’ Simba SC

Haikuwa rahisi kwa timu ya Simba SC kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Ni safari ya milima na mabonde lakini hatimaye Simba wamevuka na kuingia katika hatua ya robo fainali, na haikuwa safari ya usiku mmoja. Kauli mbiu mahususi ya ‘Do or Die’ (kufa au kupona) kama viongozi wa Simba walivyoinadi kwa mashabiki wao ilitimia, ...

Read More »

Hesabu kali zapigwa Kombe la FA

Asikwambie mtu, hakuna timu isiyopenda kuitwa timu ya kimataifa, miaka ya hivi karibuni msemaji wa zamani wa Yanga, Jerry Muro, alikuwa akijigamba kuwa timu hiyo ni ya kimataifa kwa sababu wanapanda ndege na wanashindana na timu za nje ya Tanzania. Bila kukinzana na kauli hii, timu nyingi zimekuwa katika mapambano makali ya kufanya vizuri katika fainali ya Kombe la Shirikisho ...

Read More »

Manchester United kufanya maajabu?

Kipute cha Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) wiki hii kinaendelea na leo kutakuwa na mchezo mmoja, miamba ya Hispania, Real Madrid, ikikaribishwa na timu ya Ajax katika mchezo wa marudio utakaofanyika Uwanja wa Johan Cruijjf nchini Uholanzi. Katika mchezo huo Real Madrid itamkosa beki wake kisiki, Sergio Ramos, baada ya kupata adhabu ya kadi mbili za njano katika mechi iliyopita, ...

Read More »

Simba inakula ‘viporo’

Wiki iliyopita timu ya Simba imeendelea kula viporo vyake vema katika mechi zake baada ya kuilaza timu ya Azam kwa magoli 3-1 katika Uwanja wa Taifa. Simba ilipata magoli hayo kupitia kwa Meddie Kagere aliyefunga magoli mawili huku jingine likifungwa na John Bocco, na lile la kufutia machozi la Azam likifungwa na Frank Domayo, hivyo kujiongezea nafasi ya kutwaa ubingwa ...

Read More »

Sarri bado ‘yupo yupo’

Mashabiki na wapenzi wa Chelsea wanashindwa kumuelewa Kocha wa timu yao, Mtaliano Maurizio Sarri (Garimoshi), kutokana na timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika mechi zake za hivi karibuni. Chelsea imeanza kusuasua katika mzunguko huu wa pili wa ligi katika mechi dhidi ya Arsenal, Bournemouth na Manchester City, ambapo matokeo ya mechi hizo yamewazindua mashabiki na kukosa imani na Sarri, huku ...

Read More »

Yanga yaweka ubingwa rehani

Na Khalif Mwenyeheri Yanga imeshindwa kupata matokeo mazuri katika mechi zake za hivi karibuni na kuifanya timu hiyo kupunguza nafasi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), hali hiyo inawafanya Yanga kuwa na kazi kubwa ya kufukuzia ubingwa. Katika msimamo wa ligi, Yanga inaongoza ligi baada ya kujikusanyia alama 55, katika mechi 22, huku Azam ikishika nafasi ya pili baada ...

Read More »

Ambokile amefungua njia

Mchezaji wa zamani wa Mbeya City, Eliud Ambokile (pichani), wiki iliyopita alisafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na timu ya Black Leopards inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo kwa mkopo wa miezi mitatu. Katika maisha ya soka Ambokile amepiga hatua kubwa, amefanikiwa kupata nafasi ya kucheza kwenye ligi bora licha ya kuwa na umri mdogo.   Usajili ...

Read More »

Kichwa cha mwendawazimu?

Nini kifanyike kuhusu timu za hapa nchini? Pengine ndilo linaweza kuwa swali kwa wadau wa soka. Mashindano ya SportPesa yalimalizika juzi huku tukishuhudia klabu kutoka nchi jirani zikichuana kwenye fainali. Katika mashindano hayo ambayo Yanga ilitolewa mapema tu na Kariobangi Sharks ya Kenya, hali hiyo imedhihirisha kwamba klabu za Tanzania hazijajipanga vizuri. Mashindano hayo yalihusisha timu zinazodhaminiwa na SportPesa. Wadhamini ...

Read More »

Wakati mgumu makocha EPL

Na Khalif Mwenyeheri   Ikiwa ni takriban mechi nne zimechezwa tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), hivyo kila timu ikiwa imecheza jumla ya mechi 22, huu ndio wakati ambao bodi za klabu zinazoshiriki ligi hiyo uvumilivu huwashinda. Presha inakwenda hadi kwa mashabiki ambao hawatamani kuona timu zao zikishuka daraja, maana zikishuka kurejea ligi kuu ...

Read More »

Vee Money: Aachana na Sheria, afanya muziki 

Inawezekana ukawa haufahamu historia ya msanii, Vanessa Mdee (Vee Money). Kupitia makala hii una nafasi ya kutambua alikozaliwa, alivyoanza muziki na hata mafanikio yake aliyoyapata kupitia tasnia hiyo ya muziki wa Bongo Fleva. Vee Money alizaliwa Juni 7, 1988 jijini Arusha. Ni msanii wa muziki mwenye talanta nyingi zikiwemo za kuandika nyimbo, pia ujasiriamali. Amekuwa akifahamu tamaduni mbalimbali baada ya kukua ...

Read More »

Simba kumekucha

Ni shangwe kila kona ya nchi, mabingwa wa soka wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/2018, Simba SC imetoa zawadi ya Sikukuu ya Mapinduzi kwa Watanzania. Simba imeiadhiri JS Saoura ya Algeria katika mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, mchezo huo umefanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ...

Read More »

Zahera asimamia nidhamu Yanga

Ukienda mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam yalipo Makao Makuu ya Klabu ya Yanga utawakuta viongozi, mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo hawana presha yoyote kuhusiana na mwenendo wa timu yao, wanakunywa tu kahawa. Wanaamini Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera,  ameiweka timu hiyo vizuri pamoja  na kushika usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kujikusanyia ...

Read More »

CAF yaiomba Afrika Kusini wenyeji AFCON

Karne ya 21 ina mambo mengi yanayogonga vichwa vya habari duniani, achana na kifo cha Rais wa 41 wa Marekani, George H.W. Bush, ambaye mazishi yake yamefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Achana na habari ya Bernard Membe na CCM yake, sahau kuhusu kipigo cha mbwa koko ambacho Simba SC wamewachapa Mbambane Swallows ya Swaziland na kuwasukuma nje ya mashindano ya ...

Read More »

Drogba atundika daruga

Mchezaji nyota kutoka Ivory Coast aliyeng’ara akiwa na Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Didier Drogba, amestaafu kucheza soka baada ya miaka 20 ya hekaheka uwanjani. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 40, ameichezea Chelsea mara mbili tofauti na kufunga jumla ya magoli 164 katika mechi 381. Pia ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza pamoja  na taji la Klabu ...

Read More »

Nani kuibuka mchezaji bora Afrika?

Wachezaji watano wamependekezwa kuwania tuzo ya BBC ya Mchezaji Bora wa soka barani Afrika mwaka 2018. Wachezaji wote wanacheza soka la kulipwa barani Ulaya. Wachezaji walioorodheshwa mwaka huu ni Medhi Benatia (Morocco), Kalidou Koulibaly (Senegal), Sadio Mane (Senegal), Thomas Partey (Ghana) na Mohamed Salah (Misri). Upigaji kura ulianza rasmi Novemba 17, saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki na ...

Read More »

Valencia alia na Mourinho

Nahodha wa Klabu ya Manchester United, Antonio Valencia (33), amesema Meneja wake, Jose Mourinho, amemnyang’anya kitambaa cha unahodha bila sababu ya msingi. Amesema Mourinho alisingizia kwamba yeye ni majeruhi, jambo ambalo si kweli, huku akisema huo ulikuwa ni uamuzi binafsi wa kocha wake. Amesisitiza kwamba hana jeraha lolote, bali huo ni uamuzi wake binafsi. Kwani hana jeraha lolote. Hivi karibuni Kocha wa ...

Read More »

Sanchez anatia huruma

Mshambuliaji wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza raia wa Chile, Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 29, anatajwa kutaka kuachana na klabu hiyo ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tu tangu ajiunge nayo akitokea Klabu ya Arsenal. Septemba mwaka huu Man United ilieleza nia ya kumuuza mshambuliaji huyo iwapo kiwango chake hakitaimarika. Tangu ajiunge na Mashetani Wekundu, Sanchez amekuwa ...

Read More »

Henry aizamisha Monaco?

Nahodha wa zamani wa Klabu ya Arsenal na mchezaji wa klabu za Juventus, Barcelona, Red Bulls ya New York pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa Klabu ya AS Monaco inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa. Henry ameajiriwa kwa mkataba wa miaka mitatu utakaokwisha mwaka 2021 na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Leonardo Jardim ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons