Makala

Watanzania tunaepushwa mengi

Matukio ya hivi karibuni ya nchini Sudan yanatukumbusha umuhimu mkubwa wa dhana ya kung’atuka, neno la Kizanaki lililoingia kwenye msamiati wa lugha ya Kiswahili na ambalo husikika pia kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Raia wa Sudan wamekuwa kwenye kipindi cha miezi kadhaa ya maandamano ya kushinikiza serikali yao kuachia madaraka na kuanzisha mchakato wa kurudisha utawala wa kiraia. Maandamano ...

Read More »

Haki za mtuhumiwa mbele ya polisi

Mtuhumiwa ni nani? Ni mtu yeyote anayewekwa chini ya ulinzi na polisi au chombo cha usalama kwa kutuhumiwa kufanya kosa la jinai. Makosa ya jinai ni yapi? Ni makosa ambayo mtu akipatikana na hatia hupewa adhabu. Ni makosa kama wizi, ubakaji, mauaji, kufanya makosa ya kuhatarisha amani na mengine ya namna hiyo. Haki za mtuhumiwa Mtuhumiwa anapowekwa chini ya ulinzi ...

Read More »

Ndugu Rais maneno makali ni maneno gani hayo?

Ndugu Rais, wapo wanaosema kuna maneno ambayo ni makali. Ni yapi hayo maneno makali? Ukali wake upo kwa namna yanavyotamkwa kwa ukali au ukali wake uko katika maneno yenyewe kuwa hata ukiyatamka kwa upole yanabaki kuwa makali? Kwamba, hata yakiwa yenyewe kama ni kitabuni au wapi yanakuwa makali. Maneno makali ni yapi? Ukimwambia timamu ambaye si dhaifu kuwa ni dhaifu, ...

Read More »

Epuka kuishi maisha ya majivuno (3)

Fumbua macho yako utazame. Tazama upya uhusiano wako na Mungu wako. Tazama upya uhusiano wako na mke/mume wako. Tazama upya uhusiano wako na watoto wako. Tazama upya uhusiano wako na majirani zako. Tazama upya uhusiano wako na kazi yako. Tazama upya uhusiano wako na wafanyakazi wenzako. Baada ya kutazama umebaini nini? Je, umebaini kasoro za kiuhusiano? Jifunze kumwomba msamaha aliyekukosea ...

Read More »

Kupenda si kazi, kazi ni kumpata akupendaye

Kupendwa ni mtihani.  Kupenda ni kujiweka katika hatari ya kutopendwa. Lakini hatari kubwa ni kutojiweka katika hatari. Kupenda si kazi, kazi ni kumpata akupendaye. Kuna methali ya Wahaya isemayo: “Mwereka wa mzazi unaomwangukia mtoto, si mwereka wa mtoto unaomwangukia mzazi.” Mzazi anajitaabisha kukidhi mahitaji ya mtoto, lakini baadaye mtoto hajitaabishi kukidhi mahitaji ya mzazi. Kwa msingi huu kupendwa ni mtihani. ...

Read More »

Uhuru una kanuni na taratibu zake

Uhuru ni uwezo au haki aliyonayo mtu binafsi, jumuiya au taifa ya kujiamulia mambo yake kwa hiari yake bila kuingiliwa na mtu au taifa jingine. Kuna uhuru wa mtu binafsi, ambao humpa haki ya kuishi akiheshimika sawa na watu wengine. Mtu binafsi huwa na haki ya kutoa mawazo yake, kufuata dini anayoipenda na kushiriki katika uamuzi wa mambo yote yanayohusu ...

Read More »

Yah: Mkuu, huku mbwa atamla mbwa

Kama siku zote ninavyosema salamu ni ada, na ni uungwana kujuliana hali, nawashukuru sana wote wanaonitumia ujumbe wa simu kunieleza yale ambayo yamewakuna. Hata kama litakuwa si jema kwako, naomba unijulishe ili nijue kuwa nimekukera, sisi ni binadamu, hiyo ni hatua ya maisha na lazima niipitie ili niweze kukiri, hakuna binadamu mkamilifu, karibu wote ni dhaifu. Kuimaliza wiki ukiwa salama ...

Read More »

NINA NDOTO (15)

Mambo ni mengi muda mchache   “Muda ni kitu tunachokihitaji sana, lakini ndicho kitu tuna  chokitumia vibaya,” anasema William Penn. Siku hizi ukipita mitaani utasikia watu wakisema, “Mambo ni mengi, muda mchache.” Ukweli ni kwamba mambo si mengi wala muda si mchache. “Tatizo la muda linaanzia kwenye matumizi yetu ya muda. Linaanzia kwenye vipaumbele vyetu na jinsi tunavyoutumia. Kila dakika ...

Read More »

Katika kushindwa kuna mbegu za ushindi

Ushindi ni mtihani. Si kila anayepata ‘A’ darasani atapata ‘A’ katika maisha. Si kila anayepata daraja la kwanza kwenye mitihani atapata daraja la kwanza kwenye maisha. Ushindi ni mtihani. Katika kila kushindwa kuna mbegu za ushindi, na katika kila ushindi kuna mbegu za kushindwa. Kauli hii iliwahi kutolewa na mwanadiplomasia na makamu wa 42 wa Rais wa Marekani, Walter Mondale. ...

Read More »

Ndugu Rais wanashangilia tu lakini mioyo yao haiko ‘clear’

Ndugu Rais, serikali ni sawa na mwanadamu. Haiwezekani kila kinachofanywa na serikali kikawa ni kibaya. Yako mazuri yanayofanywa na serikali. Na kuna maovu yanayofanywa na serikali. Hii ni kwa serikali zote – siyo hapa kwetu tu. Timamu hasifii kila jambo linalofanywa na serikali, na wala timamu hakosoi kila jambo linalofanywa na serikali. Timamu hushauri katika kweli na kwa nia njema ...

Read More »

DAWASA: Tunazidi kuwafikia wateja wetu

DAWASA imejizatiti katika kuhakikisha inawapatia maji salama wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na wale wa maeneo ya Mkoa wa Pwani. Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja, amekagua miradi ya maji inayoendelea kukamilishwa. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI kabla ya kuanza ziara hiyo, Mhandisi Luhemeja anasema ziara ...

Read More »

NINA NDOTO (14)

Muda ni mali, utumie vizuri   Watu wanaoishi ndoto zao ni wazuri sana katika suala linalohusu matumizi ya muda. Muda ni mali, utumie vizuri. Wakati mwingine utasikia watu wakisema muda ni pesa, lakini kwangu mimi jambo hilo ni la tofauti kidogo. Muda ni zaidi ya pesa, unaweza kupoteza pesa ikarudi, muda ukipita umepita. Hauwezi kuirudisha jana au mwaka uliopita. Kinachowafanya ...

Read More »

Kamali hatari kwa wanafunzi

Michezo ya kamali hapa nchini licha ya kuwa inaendeshwa kwa mujibu wa sheria chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), imeendelea kuathiri taifa kwa namna mbalimbali hasa vijana. Nitakijikita kwa wanafunzi ambao ndio tegemeo la taifa kuwapata wataalamu wa sasa na baadaye! Kamali ama kubeti, umekuwa mchezo maarufu zaidi kinyume cha sera ya mwelekeo wa nchi ...

Read More »

Migogoro ya TANAPA, vijiji 390 kuwa historia

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dk. Allan Kijazi, amezungumza na JAMHURI kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano. Ifuatayo ni sehemu ya pili ya mahojiano ya Dk. Kijazi na Mwandishi MANYERERE JACKTON. Endelea… Katika kuboresha uhifadhi, si tu kukabiliana na ujangili, lakini pia kuimarisha tafiti za kisayansi zinazotusaidia ...

Read More »

Vigogo wahatarisha mradi mabasi ya mwendokasi

Msongamano wa abiria wanaotumia usafiri wa mabasi ya haraka jijini Dar es Salaam maarufu kama (mwendokasi) kwa kiasi kikubwa unatokana na uzito wa kufanya uamuzi miongoni mwa watendaji serikalini. Hali ya kuchelewa kufanya uamuzi inakinzana na kasi ya Rais Dk. John Magufuli katika kutatua kero za wananchi, Gazeti la JAMHURI limebaini kuwa wakati mradi ukiwa umepangwa kuwa na mabasi 305 ...

Read More »

Huduma ya maji kumfikia kila mwananchi

Kazi zinaendelea na Wiki ya Maji 2019 imekamilika. Kitaifa Wiki ya Maji imeadhimishwa jijini Dodoma kwa wataalamu na wadau wa sekta hii muhimu kukutana na kuangalia namna bora zaidi ya kufanikisha huduma muhimu ya majisafi na salama inawafikia wananchi bila vikwazo. Matukio makubwa yanayoigusa sekta ya maji yaliyofanyika ni Kongamano la Kisayansi kuhusu sekta ya maji, Siku ya Mamlaka ya ...

Read More »

Ndugu Rais ni kweli Mtwara kuchelee?

Ndugu Rais, kwa urais wako nchini mwetu wewe ndiye baba wa sisi wote. Mwisho ni mwaka 2020 au mwaka 2025 au labda hata kuendelea, nani anajua? Marehemu mama yangu alikuwa ananiambia: “Umwenzo wa mtu inkama.’’ Maana yake: “Moyo wa mtu una siri nyingi.” Waliojibu kuwa “Mtwara kuchele” zilifanana na zile tunazozisikia tunapotembelea wodi za wagonjwa wa muda mrefu. Hawa wamekata ...

Read More »

Tunaweza kutofautisha Ujamaa na uamuzi wa busara

Mwaka 2014 nilisafiri kwa ndege nikakaa pembeni mwa abiria raia wa Kenya, ambaye alibaini nilikuwa nikisoma kitabu kimojawapo cha hotuba za Mwalimu Nyerere. Alisema: “Nasikia Nyerere aliiharibu sana nchi kutokana na itikadi yake ya Ujamaa?” Katika umri wangu nimeshasikia kwa muda mrefu maoni kama haya, maoni ambayo yamenijengea usugu wa kiasi fulani wa kutafakari hoja bila kuzingatia ni nani anayesemwa ...

Read More »

Kubadilishiwa masharti ya umiliki wa ardhi

Umiliki wa ardhi hutolewa kwa masharti maalumu. Kila aliyepewa hatimiliki anajua kuwa amepata hati hiyo kwa masharti ambayo anapaswa kuyatekeleza. Wapo ambao hudhani kuwa ukishapewa hati na masharti, basi ni hivyo hivyo tu, hauna la kufanya hata kama hujaridhika au hunufaishwi na masharti hayo. Hii ni fikra isiyo sahihi. Sasa wapaswa kujua kuwa masharti katika hatimiliki ya ardhi yanaweza kubadilishwa ...

Read More »

Epuka kuishi maisha ya majivuno (2)

Tuepuke kuishi maisha ya majivuno. Mwandishi Nadeem Kazi anatufundisha kwamba: “Hatuwezi kupanda juu kwa kuwashusha wengine chini.” Tunapanda juu kwa kuwasaidia wengine kupanda. Katika maisha lazima pia tujifunze kuwasaidia wengine. Huwezi kufanikiwa kiroho, kiuchumi, kifamilia, kiutawala, kielimu, kimaadili na kiafya kwa kuwaangusha wengine chini. Yule anayejitolea kuwasaidia wengine ndiye huinuliwa na watu aliowasaidia kuinuka. Bila shaka umewahi kujiuliza: “Kwa nini ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (24)

Moyo uliovunjika usiuvunje   Moyo uliovunjika ni mtihani. Vitu vikivunjika vinaunganishwa, si jambo jepesi kuunganisha moyo uliovunjika na kupondeka. Christie Brinkley amesema: “Afadhali kuwa na mkono uliovunjika kuliko kuwa na moyo uliovunjika.”  Moyo uliovunjika ni moyo wenye maumivu, usiuvunje. “Maumivu hayaleti jambo jipya kila mara; yakipokewa vibaya yanasababisha ulevi, weu na kujiua,” amesema Madeleine L’Engle katika kitabu chake ‘Walking on ...

Read More »

Miaka 35 bila Sokoine

Alasiri ya Aprili 12, 1984 wakati huo nikiishi Kurasini Highway, nilivuka barabara kwenda Kurasini Shimo la Udongo kuchukua picha zangu za passport kwenye studio moja. Jina la hiyo studio silikumbuki, maana miaka 35 ni mingi, lakini nakumbuka ilikuwa karibu na duka maarufu la ndugu mmoja aliyeitwa King Nose, jirani na Mti Mpana. Nilipovuka barabara na kuyakaribia maduka ya eneo hilo, ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons