Ufisadi Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro unatisha

Pamoja na malengo mengine ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), lengo mojawapo ni kuboresha miundombinu ya utalii ili kuboresha huduma za kitalii (to provide high quality tourism services) kwa kutengeneza barabara kwenda kwenye vivutio kama Nasera Rock, Olkarian Gorge na aina mbalimbali za miundombinu ya utalii na si kufanya kazi za Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Read More

Mkurugenzi: Wananchi Bukoba tulieni

*Asema ripoti ya CAG itatoa mwelekeo*Pande zinazovutana zaandaa ‘bakora’ Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Limbakisye Shimwela, amewaomba wakazi wa Manispaa hiyo kuwa watulivu na kusubiri majibu yatakayotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) baada ya ukaguzi maalum hivi karibuni. Akizungumza na JAMHURI ofisini kwake mjini Bukoba mwishoni mwa wiki iliyopita, Shimwela…

Read More

Madudu ya Msekwa yaanikwa Ngorongoro

*Aliunda Kamati ikawa ndiyo Menejimenti
*Murunya naye ahusishwa kufaidi mabilioni
*Wameuza hadi mapitio ya wanyamapori
*Faru wengine watatu hawajulikani waliko

Timu ya ukaguzi iliyoundwa kukagua ‘madudu’ katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanika ufisadi wa kutisha, JAMHURI inathibitisha. Spika wa zamani, Pius Msekwa, ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao ripoti hiyo imependekeza wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Msekwa ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo inayosifika kwa ufisadi.

Read More

IRENE DAVID: Binti aliyejiajiri kuuza matunda Dar

IRENE DAVID:

Binti aliyejiajiri kuuza matunda Dar

. Alikataa kutoa rushwa ya ngono aajiriwe

. Awaasa mabinti, wanawake wanaojiuza

 

Ni binti mrefu wa wastani, mwenye rangi ya maji ya kunde na umri wa miaka 23. Ni mhitimu wa kidato cha nne na fani ya kompyuta ngazi ya cheti, aliyejiajiri kuuza matunda. Binti huyu si mwingine yeyote bali ni Irene David, mkazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam. Ana kawaida ya kutabasamu anapozungumza na mtu.

Read More

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

‘Kutegemea kubaya kupita kote ni kutegemea mtu mwingine kwa mawazo

Katika sehemu iliyopita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema hata angekuwa anafuata sera za kibepari, angejenga viwanda. Anasema mabepari ndiyo walioanza kujenga viwanda, na viwanda vyenyewe havikuwa na sera. Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mwalimu aliyoitoa katika kilele cha Sherehe za Mei Mosi, mwaka 1995 mkoani Mbeya.Juzi

Read More