Mwanamuziki Naseeb Abdul, maarufu Diamond Platnumz amemtumia salamu za pongezi mwanamuziki mwenzake, Ali Saleh Kiba maarufu Alikiba kufuatia kufunga ndoa leo Aprili 19.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa anampongeza King Kiba kwa kuoa na kumtakia maisha mema ya ndoa.

“Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo…Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele…”

Watu wamekua na maoni mbalimbali kufuatia hatua hiyo, kutokana na hali inayoamini kuwa wawili hao wamekuwa na hali ya kutokuelewana kwa muda mrefu.

Alikiba amefunga ndoa leo mjini Mombasa Kenya na mchumba wake Aminah Rekish ambapo harusi yake imefanyika huko lakini pia inatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

1592 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!