Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally kwenye meza kuu mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwa meza kuu mara baada ya kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally wapili kutoka kulia kwenye meza kuu kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa NEC hawaonekani pichani, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe mara baada ya kikao cha NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bashiru Ally amepitishwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.
Dkt. Bashiru amepitishwa leo Mei 29, 2018 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama(NEC)

Dkt. Bashiru ni Mwalimu Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia alikuwa Mwenyekiti wa Tume maalum ya kuchunguza mali za CCM iliyoundwa na Rais Magufuli

PICHA NA IKULU

1884 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!