Staa wa Bongo katika muziki wa kizazi kipya Aslay Isiaka, ‘Dogo Asley’ ambaye makazi yake ni jijini Dar es Salaam amesema kuwa sasa anfurahia maisha ya muziki kutokana na maendeleo aliyoyapata.

Msanii huyo ambaye  alifahamika haraka kutokana na kibao chake cha ‘Naenda  Kusema Kwa mama’ amesema kuwa sasa ana imani kwamba anauwezo wa kufanya mambo ya maendeleo katika maisha yake kupitia muziki.

 

Mwanamuziki huyo alisema kuwa kwa sasa anafanya muziki lakini pia anazingatia suala la masomo. “Kwa sasa nafanya muziki vile vile ninasoma kwahiyo naamini kuwa hapo baadaye naweza kufanya vitu vya maana zaidi katika maisha yangu,” Alisema mwanamuziki huyo.

 

Moja ya mambo ambayo mwanamuziki huyo ameyafanya  tangu ameingia rasmi katika muziki yapata miaka mitatu iliyopita  ni pamoja na kuwajengea nyumba wazazi wake katika eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. Halikadhalika kwa sasa anaendelea na masomo.

 

Baada ya kufanya vizuri na kibao chake cha kwanza cha ‘Naenda Kusema kwa Mama’, kinda huyo alipokelewa vizuri na washabi wa muziki wa kizazi kipya. Hali hiyo ilimpa hamasa ya kuendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya akiwa na kundi la TMK Wanaume chini ya usimamizi wa Said Fella.

 

Nyimbo nyingine ambazo zimefanywa na mwanamuziku huyo ni pamoja na Bado Mdogo aliomshirikisha mwanadada Estelina Sanga ‘Lina’, Maneno Ya Wahenga, Umbea aliomshirikisha Chege na  na Niwe Nawe.

 

Msanii huyo alitambulishwa rasmi katika anga za muziki Oktoba 31, 2012 katika  na kundi la Mkubwa na Wanawe linalomilikiwa na Said Fella katika viwanja vya Sigara Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

 

0783 106 700


By Jamhuri