HATMA YA RAIS JACOB ZUMA KUNG’ATUKA MADARAKANI KUJULIKANA LEO

Kiongozi wa Chama Tawala nchini Afrika kusini Cyril Ramaphosa
Kiongozi wa Chama Tawala nchini Afrika kusini Cyril Ramaphosa

 

Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma.

Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu.

Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.

Bwana Ramaphosa alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 28 toka Rais wa kwanza mzalendo nnchini humo Nelson Mandela alipolihutubia taifa, mara tu baada ya kuachiwa gerezani.