Spika Job Ndugai amelieleza Bunge kuwa matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, tundu Lissu (CHADEMA) aliyeko hospitalini nchini Ubelgiji yanagharamiwa na serikali ya Ujerumani.

Ndugai alisema amefahamu hilo kwa kupewa taarifa na Balozi wa Ujerumani nchini, Dkt Detlef Weacter lakini pia akataja masharti matatu yanayopaswa kusingatiwa ili Bunge ligharamie matibabu yake hayo ughaibuni.

Lissu (50), anaendelea na awamu ya pii ya matibabu yake ya kibingwa nchini Ubelgiji baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa anajiandaa kushuka kwenye gari nyumbani kwake Area D mjini Dodoma, Septemba 7, 2017.

Matibabu ya Mbunge huyo yalianzia kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma kabla ya Mnadhimu huyo wa Kambi ya Upinzani kuhamishiwa katika Hospitali ya Nairobi, Kenya.

CHADEA na familia yake wamekuwa wakilalama serikali kukataa kugharamia matibabu ya mbunge huyo ambayo ni “haki yake ya msingi”, ikiwemo jana bungeni.

Hata hivyo, Spika Ndugai alilieleza Bunge haliwezi kulipa gharama za matibabu ya Lissu kwa kuwa hayakufuata taratibu za nchi ambazo wabunge na raia wa kawaida wanapaswa kuzifuata ili serikali igharamie matibabu yao nje ya nchi.

Spika Ndugai alilazimika kutoa ufafanuzi huo bungeni Dodoma, kutokana na mwongozo ulioombwa kwake na Godbless Lema.

Mbunge wa Arush Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), alitaka uongozi wa Bunge ueleze kwanini chombo hicho cha kutunga sheria hakitaki kugharamia matibabu ya Lissu.

Katika kujenfa hja yake, Lema alisema Lissu ana haki za kibunge na za raia wa kawaida kulipiwa gharama za matibabu na serikali ilivyofanyika kwa Spika Ndugai ambaye ana siku chahe tangu arejee nchini akitokea kwenye matibabu ya muda mrefu nchini India.

By Jamhuri