John Bocco, amesema Lipuli ijiandae kupokea kipigo kwa kuwa lengo lao kubwa ni kupata ubingwa.

Mchezaji huyo ambaye jana alifunga bao la kwanza wakati Simba ikiifungaTanzania Prisons Uwanja wa Taifa, amesema mechi na Lipuli si ya kubeza lakini sisi tupo vizuri.

Bocco ameeleza kuwa wanaijua Lipuli vizuri na watacheza kwa kujituma ili kupata matokeo waweze kutenegeza mazingira mazuri ya kuwa bingwa msimu huu.

Simba Sc walifanikiwa kuifunga Prisons mabao 2-0 jana na kufikisha alama 58 kileleni.

Simba itashuka Uwanja wa Samore Aprili 21 Jumamosi ya wiki ikiwa mgeni wa Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

1370 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!