“Pamoja na kwamba mimi binafsi napenda tuendelee kufundisha Kiingereza katika shule zetu, kwa sababu Kiingereza ndicho Kiswahili cha Dunia, tuna wajibu mkubwa kuzidi kukiendeleza na kukiimarisha Kiswahili: Ni silaha kubwa ya umoja wa Taifa letu.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, yanayopatikana katika moja ya hotuba zake kwa umma. Alizaliwa Aprili 13, 1922 kijijini Butiama, Mara na kufariki Oktoba 14, 1999 jijini London, Uingereza.

Malkia Elizabeth II: Natangaza wakfu

“Ninatangaza mbele yenu wote kwamba maisha yangu yote, iwe ni muda mrefu au mfupi, yatakuwa wakfu ya kuwahudumia.”

Hii ni kauli ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza, wakati akisisitiza kuwahudumia wananchi kwa uzito unaostahili. Alizaliwa Aprili 21, 1926 huko Mayfair, jijini London, Uingereza.

 

Wangari Maathai: Tuhifadhi mazingira

“Tuna deni kwetu wenyewe na kwa kizazi kijacho la kuhifadhi mazingira ili tuweze kuwarithisha watoto wetu Dunia endelevu inayonufaisha wote.”

Haya yalisemwana na mwanaharakati maarufu wa mazingira na siasa wa nchini Kenya, Wangari Maathai, katika harakati zake za kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo. Alizaliwa Aprili 1, 1940 kijijini Tetu na kufariki Septemba 26, 2011 jijini Nairobi, Kenya.

 

Saddam Hussein: Mungu ni mshindi

“Wote wanaopigana kwa sababu ya Mungu watakuwa washindi.”

Rais wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, aliyanena haya kukumbusha kuwa siku zote wapiganaji wanaotetea haki, Mungu huwajaza uwezo wa kuwashinda maadui zao. Alizaliwa Aprili 28, 1937 huko Al-Awja na kuuawa kunyongwa Desemba 30, 2006 jijini Baghdad, Iraq.

 

 

 

 

 

By Jamhuri