Mimi Baraka Mukundi, mkazi wa Arusha niliajiriwa na Kanisa la Wasabato Makao Makuu Arusha, Tanzania mwaka 1986. Niliendelea kufanya kazi na kanisa hilo katika vitengo vyake mbalimbali kwa kadri walivyokuwa wakinipangia kazi kulingana na taratibu za Kanisa za ajira. Kipindi cha mwaka 1999 nilihamishiwa katika kiwanda kilichokuwa kinamiikiwa na kanisa, kilichojulikana kama INTERNATIONAL HEALTH FOODS OF SDA CHURCH, ambacho kilikuwa kikizalisha vyakula vya lishe.

Nilifanya kazi katika kitengo hicho cha kanisa hadi Novemba, 2002 ajira yangu ilipositishwa kwa maneno ya mdomo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bwana Jose Luis Gomez Bayo. Hali hiyo ilinilazimu kwenda kwenye Baraza la Usuluhishi Arusha kutafuta usuluhishi. Ilipofika Juni 2, 2004 Baraza la usuluhishi Arusha liliamuru nirudishwe kazini na kulipwa haki zangu stahiki. Nakala ya uamuzi huo wa Baraza la Usuluhishi ninazo.

International Health Foods of S.D.A Church, bila kuzingatia hitaji la kutekeleza uamzi huo wa Baraza la usuluhishi, kwa kumtumia wakili wao, MARO AND COMPANY ADVOCATES, ARUSHA, walikwenda Mahakama Kuu, Arusha kupinga uamuzi wa Baraza la Usuluhishi. Maombi hayo Misc. CIVIL CAUSE NO. 12 OF 2004 yalitolewa uamzi na Mahakama Kuu, Arusha, tarehe 13 Februari, 2009 kwa Mahakama Kuu kuyatupilia mbali maombi hayo pamoja na gharama. Nakala ya uamuzi huo wa Mahakama Kuu, Arusha ninazo.

Kutokana na uamzi huo wa Mahakama Kuu, Arusha, nilirejea tena kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ili kuendelea na utekelezaji wa maombi yangu Na. 19 ya 2008. Nilikubaliwa kuendelea na utekelezaji huo kama ilivyokuwa amri. Nakala ya uamzi huo pamoja na Amri hiyo ya utekelezaji ninavyo.

Katika ombi hilo Na. 19 ya 2008 la utekelezaji wa Amri hiyo ya Mahakama iliyotolewa tarehe 1 Aprili, 2008, Mahakama iliamuru mali ya mdaiwa (International Health Foods of S.D.A. Church) kukamatwa kama ilivyokuwa imeombwa. Amri hiyo ya Mahakama iliyopo kwenye mwenendo wa shauri Na. 19 ya 2008, ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi tarehe 1/4/2008.

Amri hiyo ikiwa bado haijaondolewa, wakati wakili wa International Health Foods of S.D.A Church akiomba Mahakama kupewa muda wa kuleta utetezi ili kubatilisha uamuzi wa kukamata mali ya Mdaiwa, kwa makusudi International Health Foods of S.D.A Church, walipuuza amri halali ya Mahakama na kuingia Mkataba wa Mauzo wa mali ya Mdaiwa iliyokuwa imekamatwa na kuiuza kwa siri kwa JAMAHEDO HEALTH FOODS COMPANY LIMITED tarehe 25 Julai, 2008.  Nakala ya Mkataba huo wa mauzo ambao fedha zake zilihamishwa kupitia Benki ya CRDB, Tawi la MERU, ninavyo.

KATIKA Mkataba huo wa Mauzo unaelezea mambo yafuatayo:-

“CONSIDERARTION: USD 900,000 (UNITED STATES OF AMERICA DOLLARS, NINE HUNDRED THOUSAND ONLY payable upon execution hereof. But it should be pointed out here that, the vendor shall execute this Deed immediately after the whole amount to the Tune of USD 900,000/= has been deposited in the Account of General Conference of SEVENTH DAY ADVENTIST vide Account Na 5300375704. PNC BANK, THE NPC FINANCIAL SERVICE GROUP USX TOWER, 600 GRANT STREET, MAILSTOP P6- PUSX – 361, PITTSBURG ABA – 031D00053”

Mauzo hayo ya mali isiyohamishika ya mali Mdaiwa, yalifanywa kwa nia ovu na hasa ukizingatia makusudi na misingi ya uanzishwaji wa kiwanda hicho ambayo yameainishwa kwenye TRUST DEED OF INTERNATIONAL HEALTH FOODS OF S.D.A. CHURCH, iliyoandaliwa na HOSEA & COMPANY ADVOCATES OF P.O.BOX 12745 DAR- ES – SALAAM, ambayo sehemu ya maelezo katika Sura ya 8.1 yanasomeka kama ifuatavyo:-

 “8. DISSOLUTION

The Trust shall endure for an indeterminate period but may be dissolved by a resolution of two third of the Trustees in a meeting convened to discuss the dissolution and in such event the assets belonging to the Trust shall be realized and handed over by the Trustees to the Seventh Day Adventist Church in Tanzania.

Nakala za vibali vilivyoombwa na Kanisa kwa ajili ya uanzishwaji wa kiwanda hicho cha Kanisa ninavyo.

Nakala ya Barua ya utambulisho inayokitambulisha Kiwanda hicho  kama kiwanda cha Kanisa la Wasabato ikiwa imetumwa kutoka Seventh Day Adventist Australia tarehe 1 Novemba , 1999.

International Health Foods of S.D.S Church, wakiwa wamejiridhisha kwamba jambo hilo ni la siri, siwezi kufanikiwa kupata haki yangu baada ya kuhamisha fedha zote za mauzo ya mali isiyohamishika ya Mdaiwa na kuzipeleka Makao Makuu ya Kanisa Marekani isivyo halali, tarehe 12/8/2009 walikula njama wakishirikiana na mnunuzi wa mali hiyo haramu aitwaye JAMAHEDO HEALTH FOODS COMPANY LIMITED na kisha kwenda Mahakamani kufungua kesi No. 42/2009 huku wakiambatanisha Mkataba wa uongo walioubuni ili kupotosha ukweli, huku wakijua haikuwa kweli, Mkataba huo unaodaiwa kufanywa na KAMPUNI YA JAMES JOHN MWALEX COMPANY ADVOCATE, INDIA STREET, P.O.BOX 2122, ARUSHA, unadaiwa kufanyika tarehe 26 Mei, 2008. Katika Mkataba huo wa Mauzo uliowasilishwa Mahakamani kama kielelezo JJM 1 unasomeka kama ifuatavyo:-

“CONSIDERATION: TANZANIA SHILLING NINETY MILLION ONLY (TZS 90,000,000/=) , payable upon execution hereof  But  it should be pointed out here that, the vendors shall Execute this Deed immediately after the whole amount to the Tune of TZS. 90,000,000/= has been deposited in the Account of General conference of SEVENTH DAY ADVENTIST vide Account No. 530037574, PNC BANK, THE NPC FINANCIAL SERVICE GROUP USX TOWER, 600 GRANT STREET, MAILSTOP P6 – PUSX – 361, PITTSBURG ABA – 031D00053

 SCHEDULE “A”.

THAT  the following facts were extracted from the Valuation Report which was conducted on the 16th Day of June, the Year , 2008 by KNIGHT FRANK – DAR ES SALAAM and the same given to us by the Management of International Health Food Association (IHFA). The said Report was given to JAMAHEDO Company ltd, as a Company which won the tender, on the 24th Day of July, the Year, 2008

Maswali ya kujiuliza ni kwamba, kama International Health Food Association waliingia Mkataba wa mauzo tarehe 26 Mei, 2008, tathimini iliyofanywa na Kampuni ya KNIGHT FRANK – DAR ES SALAAM tarehe 16 June, 2008 ilikuwa ikikihusu kiwanda gani? Swali jingine ni kwamba Kampuni ya JAMAHEDO walitangazwa kuwa washindi wa tenda hiyo ya ununuzi wa Kiwanda tarehe 24 Julai, 2008.  Je, tarehe 26, Mei, 2008 walipoingia Mkataba wa kununua kiwanda, walikuwa wananunua kiwanda kipi kama walikuwa tayari wamekamilisha malipo tarehe 26 Mei, 2008?

International Health Foods of S.D.A Church, wakidhamiria kuendelea kuzuilia haki iliyokwisha amriwa, wakiwa wamekiuka amri halali ya Mahakama, walirudi tena kwa mara nyingine katika Mahakama Kuu na kufungua shauri jingine katika Misc. CIVIL APPLICATION NO. 69 OF 2009, shauri ambalo hawakufanikiwa kutokana na misingi ya kisheria. Nakala ya uamuzi wa Mahakama ninayo.

Wakiendelea kuthibitisha kwamba nia yao haikuwa njema, badala ya kutekeleza uamuzi huo halali wa Mahakama na wakidhihirisha kwamba hawakuwa tayari kutekeleza uamuzi huo wa Mahakama, walirudi tena Mahakama Kuu Arusha tarehe 23 Oktoba, 2009 kupitia kwa wakili wao aliyeiandikia Mahakama Kuu, Arusha barua akiomba lifunguliwe shauri jingine, na kutokana na barua hiyo Mahakama Kuu ikafungua Shauri CIVIL REVISION NO. 7 OF 2009. Shauri hilo lilifunguliwa kwa maombi ya barua ya Mdaiwa, yalitolewa uamuzi na Mahakama Kuu, Arusha tarehe 22/04/ 2010 na mimi kupewa ushindi, wakati Mahakama ikizitupilia mbali hoja za Mdaiwa.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu Arusha, haujawahi kupingwa na Mdaiwa wala kukatiwa Rufaa katika Mahakama yoyote nchini tangu ulipotolewa  hadi leo. Kutokana na Kiwanda hicho kumilikiwa na Kanisa la Seventh Day Adventist Church Tanzania, ambaye pia ndiye mwajiri wangu, nimejaribu kufuatilia haki zangu kupitia kwa wakili wangu aliyejitolea kunisaidia kwa sababu yangu kukosa fedha, lakini juhudi zote zimekuwa bila mafanikio kwa madai kwamba wao Seventh Day Adventist Church Tanzania, wameiachia General Conference of S.D.A Church Marekani ili ndio washughulike na jambo hili. Wakili wangu pia amejaribu kuwasiliana na General Conference of SDA Church Marekani, ili kufuatilia haki zangu lakini pia wamekuwa kimya baada ya kutumiwa nyaraka zenye ukweli husika. Nakala ya Mawasiliano ya wakili wangu Mhe. Anthony Rutabanzibwa na General Conference of Seventh Day Adventist Church Marekani kwa njia ya e-mail vipo.

Kwa vielelezo nilivyo navyo, hajawahi kutokea kiongozi yeyote kutoka General Conference of S.D.A. Church Marekani na kuja nchini Tanzania ili kuomba vibali kwa ajili ya kuanzisha Kiwanda hicho nchini. Vibali vyote vilivyoambatanishwa viliombwa na Makao Makuu ya Kanisa la Wasabato Tanzania ambao waliithibitishia serikali kwamba kiwanda hicho ni mali ya Kanisa la Wasabato Tanzania, na nyaraka zote zinathibitisha hivyo pamoja na namna wanavyohusika. Inaleta ukakasi leo ninapodai haki zangu baada ya wao kula njama na kupeleka fedha za mauzo ya mali inayodaiwa Marekani halafu  wadai wanawaaachia  General Conference of SDA Marekani ndio washughulike na shauri, na hili ni  kwa vile wanajua sina uwezo wa kwenda kudai Marekani. Katika Working Policy ya kanisa, SEVENTH DAY ADVENTIST CHURCH WORKING POLICY – EAD POLICY.

SECTION O – GENERAL ADMINISTRATIVE POLICIES iko wazi nayo inasema yafuatayo:-

 

 GENERAL ADMINISTRATIVE POLICIES

* 01 20 General Conference – The General Conference is the largest Unit or Organization embracing all Union Conferences Union missions and other church Organizations in all parts of the World.

Division Sections – As provided by its Constitution and Bylaws the General Conference conducts its work in division sections. Each division section operates within a specific territory in harmony with General Conference policies. A division section embraces all the local or Union / fields in its assigned area of the world.

 EAD POLICY

“G  45 PLAN OF OPERATION OF HEALTH – CARE INSTITUTIONS

G 45 10 GOVERNANCE – 1. Ownership conditions which may vary from institution to institution or from country to country may prohibit rigid adherence to an international pattern, but they shall in general include the following provisions.

Ownership shall be vested in a specific church entity.

No Indicia of ownership shall be present to unless the church exercises ultimate control of an Organization.

Equipment may be owned or leased.

The buildings and land shall be titled by church or secured by a lease of at least 25 years.

The use of the property shall be assured on a continuing basis over an extended period of time, and the church shall have full responsibility for policies, administration, finance, and freedom to operate the institution according to Seventh Day Adventist belief and standards.

Nakala ya maelezo ya EAD Working Policy na makala iliyoandaliwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Wasabato Tanzania kwa wakati huo (Tanzania Union of SDA Church) Pastor. Stephen M. Bina, maelezo aliyoyatoa wakati wa sherehe ya Kanisa la Wasabato Tanzania kutimiza miaka 100, ninavyo.

Je, Kanisa lilidanganya wakati wa uombaji vibali serikalini kwa ajili ya uanzishwaji wa kiwanda hicho, ama kulikuwa na kikundi tu cha watu kilichotumia kivuli cha Kanisa katika kuanzisha kiwanda hicho cha International Health Foods of S.D.A. Church, wakitumia mwanya huo ili kuficha maovu yao?

Na kama ndivyo, iliwezekanaje fedha ya mauzo hayo haramu ya mali isiyohamishika ya Mdaiwa ihamishiwe kwenye Akaunti ya Kanisa la Wasabato Makao Makuu Marekani, halafu na wao wakae kimya na fedha hizo ambazo hazikuwa za Kanisa?

Naamini jambo hili ni lile walilokubaliana ili kuendelea kuzuia haki iliyokwisha amriwa na Mahakama. Je, kama uamzi wa Mahakama hauwezi kuheshimiwa, ni wapi haki itakapopatikana?

Niliajiriwa na Kanisa la Wasabato Makao Makuu Tanzania mwaka 1986, waliniajiri kutokea nyumbani kwetu mkoani Mwanza, Wilaya ya Ukerewe, na nimelitumikia Kanisa kwa miaka zaidi ya 17 kama mwajiriwa. Lakini tangu mgogoro huo ulipoanza Novemba 2002, mwajiri wangu amekaa kimya bila kujua ninakula nini pamoja na familia yangu, wala hajui ninapoishi baada ya kunifukuza kwenye nyumba aliyokuwa amenipangishia.

Kulingana na Sheria ya Usalama Kazini Na. 62 ya 1964 alipaswa kunilipa nusu mshahara wakati shauri hilo likiendelea kutafutiwa ufumbuzi katika Mahakama, lakini mwajiri wangu amenitelekeza pamoja na familia yangu tangu Novemba, 2002 bila kunipatia aina yoyote ya msaada au pesa yeyote ya kujikimu kwa kipindi chote hicho.

Badala yake alinifukuza ndani ya nyumba aliyonipangishia pamoja na familia yangu na hivyo kuniacha nihangaike mitaani katika Jiji la Arusha. Nakala ya barua za kufukuzwa kwenye nyumba pamoja na nakala ya haki za Mwajiriwa wa kanisa la Wasabato nimeziambatanisha.

Hali hii ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hali ambayo imeifanya familia yangu kuathirika kwa kiwango cha kutisha kisaikolojia. Watoto wangu wamekuwa wakihangaika kwa kukosa mahitaji yao muhimu ikiwa ni pamoja na kuachishwa masomo yao mara kwa mara kwa kukoswa ada, hali inayowasabisha wasifanye vizuri katika masomo yao, na hivyo kuwafanya wakose uhakika wa maisha yao ya baadaye, huku haki ya utumishi wangu ambayo ni haki ya wanangu ikizuiliwa isivyo halali na mwajiri wangu.

Athari mbaya za wazi ni pamoja na hii ambayo imemtokea mwanangu mwenye mahitaji maalumu aliyekuwa akipatiwa huduma muhimu ya matibabu kutoka kwa mwajiri kutokana na utumishi wangu, alikuwa akihudumiwa na madaktari katika hali yake waliyoamini kwa kuendelea kumpatia huduma hiyo angeweza kutembea mwenyewe, lakini kutokana na mwajiri wangu kusitisha huduma hiyo muhimu pamoja na  mshahara wangu huku akiniacha bila ya aina yoyote ya msaada, hali hiyo imemwachia mwanangu ulemavu wa kudumu na kusababisha machungu ambayo ni machungu hata kuyaeleza.

Hali hii inatisha na kusikitisha katika namna ambayo hata siwezi kupata maneno ya kueleza. Nakala ya   picha za mwanangu alipokuwa akihudumiwa na mwajiri tangu utoto wake hadi leo nimeziambatanisha.

Ni katika mazingira haya ya unyanyaswaji na uonevu wa wazi unaofanywa dhidi yangu na familia yangu isiyokuwa na hatia, familia ambayo imeendelea kuishi kama omba omba katika Jiji la Arusha, ninapolazimika kuomba msaada wa kiutawala ili kusaidia kuipata haki iliyozuiliwa kimabavu isivyo halali wakati shauri lilikwisha kamilika mahakamani, na kukiwa hakuna shauri jingine lolote liliofunguliwa kupinga uamuzi huo wa Mahakama.

Kama mzazi mwenye uchungu na familia yangu kwa muda mrefu imenilazimu kukimbia huku na kule nikihangaika kwa ajili ya kuisaidia familia yangu, na hivyo kukaa mbali na familia; jambo ambalo limeiathiri familia yangu kwa kiasi kikubwa na kuifanya ionekane haina maana katika jamii inayotuzunguka. Hadi sasa nadai Sh 2,408,172,436.91.

Natanguliza shukrani zangu za dhati nikiamini nitasaidiwa jambo hili kwa haraka kwa kadri Mungu atakavyojalia ili kuinusuru familia yangu ambayo imeendelea kunyanyasika wakati haki yangu ikiwa imezuiliwa isivyo halali na kusababisha kukosa mwelekeo.

 

Mwenye kuguswa na taarifa hii, au mamlaka iliyo tayari kumsaidia inaweza kuwasiliana na Mhariri wa Habari wa JAMHURI kwa namba 0765791573

1864 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!