KATAMBI AELEZEA SABABU ZA KUYUMBA KWA CHADEMA

KADA mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ameeleza sababu zinazochangia kudhoofika kwa vyama vya upinzani nchini.

Amesema kuyumba kwa vyama hivyo kunachangiwa na ubinafsi waviongozi wake ambao wengine wageuza Chama ni mali yao na kutoamaamuzi ambayo si shirikishi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Katambi amesema kuwa tanguameondoka Chadema ambako alikuwa Mwenyekiti wa Vijana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amekuwa kimya muda mrefulakini ameona ni vema akasema mambo kadhaa kuhusu hali ya kisiasa nchini.

Kuhusu vyama vya siasa kuyumba, Katambi amesema zipo sababuambazo zimekuwa zikichangia vyama hivyo kushindwa kuwa imara namatokeo yake kubaki kulalamikia kila jambo ambalo linafanywa naSerikali hata liwe lenye maslahi kwa nchi.

“Upinzani umeshindwa kujenga chama taasisi kwani hivi sasa kilachama ni cha mtu.vyama vingi ni vya watu na si taasisi.Dhana yataasisi ni kwamba sheria ,kanuni na taratibu lazima zifuatwe”Kama mtu anadharau katiba na misingi iliyowekwa basi huo niudikteta. Wapinzani kabla ya kukimbilia kugombea udiwani na ubunge wajikite kwanza kujenga taasisi, kama wameshindwa kuheshimu katiba za vyama vyao wanapate uhalali wa kudai Katiba,”amesema.

Amesema sababu nyingine vyama vya upinzani vimekosa uamuzi shirikishi.”Chadema ambayo inajieleza ni chama cha upinzani chenye nguvukimeshindwa kuwa na utaratibu wa kuwa na maamuzi shirikishi nahata yanayoamriwa ni maamuzi ya mtu.Na pia kuna ukiukwaji wauteuzi wa nafasi ikiwamo za ubunge viti maalumu ambao umetawaliwana rushwa na kupeana nafasi kirafiki.

“Tatizo la upinzani hakuna kuheshimiana na ukosefu wa maadili yaviongozi. Kama Taifa lazima liwe na viongozi wanaozingatia maadili,kwa mfano leo hii Ukawa wakichukua nchi nani anaweza kuwa WaziriMkuu,”amesema.

Kada huyo wa CCM, amesema kuwa vyama vya upinzani adui yaomkubwa ni CCM lakini wameshindwa kuwa na uwazi kwenye mali zaokwani hata Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),akikagua ni lazima atapata hati zenye shaka kwani fedha za ruzukuzinatumika vibaya.

“Wanaosema nimenunuliwa wanajidanganya kwani wakati anakwendachadema wamemnunua kwa shilingi ngapi. Kuna wabunge zaidi ya 15wataondoka Chadema na kuna wajumbe wapo ndani ya chama hicholakini tayari wameshaondoka ila wanaingia kwenye vikao ili kutimizawajibu tu,” amesema Katambi.

Amesema kwa sasa vyama vya upinzani wamekosa ajenda na waliopo huko wanakwenda tu bora liende na wengine wanajua wakitoka hawataajirika.”Kukosea ajenda chadema walikuwa wanasema wanapambana naufisadi na hata slaa aligeukwa kwa sababu ya masilahi ya watu binafsi.Chadema ya Dk. Slaa kila mtu anaifahamu ilifika wakati akapelekwaMarekani kwa ajili ya kuandaliwa ili aje kuwa Rais lakini baadaye wakaanza kumtuhumu kwa usaliti,” amesema

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa sasa umefika mwisho wa Umojawa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwani malengo ya Chademayametimia kwa kuua nguvu ya kila chama ili wabaki wao katikaupinzani.