Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akifuatilia kikao na Kikosi kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi, leo mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiongoza kikao na Kikosi kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura walipokutana leo mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.
Mkurugenzi Idara ya Sera na Bunge Ofisi ya Waziri Mkuu,Yona Mwakilembe akitoa ufafanuzi katika kikao hicho wakati Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kilipokutana na Katibu Mkuu (hayupo pichani) leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura wakifuatilia kikao na Katibu Mkuu (hayupo pichani) leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.
 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni Taasisi mojawapo iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi amekutana na Kikosi Kazi cha Tume hiyo kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma, lengo ni kuangalia namna serikali inavyoweza kusaidia kwa maeneo inayoruhusiwa kikatiba katika kuwasaidia kutekeleza majukumu yake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 5 kifungu kidogo cha 3 (a) ambacho kimeweka uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini na Ibara ya 74 kifungu kidogo cha 6 (a) na (e), kinaipa Tume madaraka ya kuchukua jukumu la kuandikisha wapiga Kura nchini Tanzania.
Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 15 (3) kinaipa madaraka Tume ya Uchaguzi kutengeneza mfumo na utaratibu wa uandikishaji wa wapiga Kura nchini na uboreshaji wa daftari hilo mara mbili kati ya Uchaguzi mkuu mmoja na unaofuata.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni miongoni mwa Taasisi ambazo zipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi hiyo ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
 
1349 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!