Mwanahabari mwandamizi na katibu mkuu wa zamani wa TFF, Angetile Osiah amenusurika kifo katika ajali mbaya ya gari, jana.
Osiah alipata ajali mbaya baada ya gari lake kugonga roli akiwa njiani kwenda nyumbani kwake Chanika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Angetile ambaye mmoja wa waandishi na wahariri bora wa habari za michezo nchini alisema alikuwa njiani kurejea nyumbani.
“Ilikuwa kama muda wa saa 3 usiku. Nikiwa nyuma, roli lilisimama ghafla mlimani, nikalivaa kwa nyuma. Nimeumia hasa mdomo, lakini naendelea vizuri,” alisema.
Baadaye alikimbizwa hospitali na kupatiwa matibabu na baadaye ilielezwa kuwa anaendelea vizuri.
 
Imeelezwa Osiah alikuwa akitoka ofisini kwake Mwananchi eneo la Tabata jijini Dar es Salaam.
928 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!