Spika anachangia fujo bungeni

Fujo bungeni zinachangiwa na Spika Anne Makinda kutosimamia vizuri haki, kanuni na sheria za Bunge. Hataki wabunge wa kambi ya upinzani wawakosoe wabunge wa chama tawala. Hii haileti ladha.

Mdau wa JAMHURI, Dodoma

Watumiaji wa simu tumeliwa

Nchi hii ni ya ajabu sana, walitudanganya gharama za kupiga simu zitashuka lakini hakuna kitu, tunaona vipromosheni uchwara tu. Kila siku tunaambiwa “Jiunge.” Tumeliwa!

Msomaji, Dar


Tusiuchafue mji wa Kataru

Wakazi wa Karagwe tuwe wastaarabu kwa kutunza mandhari ya mji huu. Ni aibu kwa mji huu wenye wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi kuwa mchafu.

Msomaji wa JAMHURI, Karatu

 

SUMATRA imulike daladala hizi

SUMATRA mnakaa tu ofisini. Wakazi wa Kinyerezi, Dar es Salaam tunanyanyaswa na daldala za Ubungo, zinaishia Segerea. Fuatiliani pale Segerea Mwisho mwone maajabu ya hizo daladala.

Mpenzi wa JAMHURI, Dar

 

Pongezi JAMHURI

Pongezi Gazeti la Jamhuri, nawapongeza sana kwa kazi yenu nzuri ya kutuletea habari za uhakika, zilizochambuliwa kwa kina. Vilevile maandishi yanaonekana vizuri, tunasoma bila miwani. Hongereni sana.

Charles R. Mwanjelwa, Kyela.

 

Ndalichako ajiuzulu Elimu

Serikali imefuta matokeo ya kidato cha nne 2012, hatua hiyo pekee haitoshi, na yule mama Ndalichako ajiuzulu. Ugumu uko wapi? Mbona Lowassa na Mwinyi walijiuzulu kwa kashfa za kiutendaji.

Mbonde Ngungane, Kibaha

 

Polisi, Spika watende haki

Jeshi la Polisi – Idara ya Usalama wa Taifa na Spika wa Bunge wasikandamize demokrasia nchini, watende haki kwa watu wote kwa manufaa ya Watanzania.

Josephat Manyeye, Chato

 

Mhandisi Misenyi anatukera

Mhandisi wa ujenzi Wilaya ya Misenyi ni kero kwa wafanyakazi wenzake na wakandarasi, anatuumiza. Mamlaka husika itutatulie kero hii.

Msomaji, Misenyi – Kagera

 

Wastaafu watakumbukwa lini?

Wastaafu wa UDSM ni kama wastaafu wa EAC mwaka 1977, huu ni mwaka wa 36 bado wanapigwa danadana. Watapigwa danadana hadi lini?

Mzee mstaafu, Morogoro

1146 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!