Stendi ya Nyegezi ni jehanamu

Stendi ya mabasi ya Nyegezi, Mwanza ni mithili ya jehanamu, utapeli na usumbufu vimekithiri. Kwanini stendi za Tanzania zimeachwa kuwa vituo vya uhalifu wa kila aina, huku polisi wapo? Uchunguzi zaidi ufanyike kusaidia wananchi.

Rwambali F, Mwanza

Tusikurupuke kurudia mtihani

Tume ya uchunguzi isikurupuke kurudia mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012. Je, wanafunzi waliojiua watafufuliwa? Je, waliokwishalipia ada za vyuo? Au ni kutaka kutoneshana vidonda?

Msomaji wa JAMHURI, Dar

 

Tuliwatuma kufanya ngono zembe?

Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya inapoomba ipewe Sh milioni 18 kwa ajili ya wajumbe watakaougua ukimwi ni hatari sana! Ina maana Watanzania waliwatuma kwenda kufanya ngono zembe?

Dk. Nabwera, Arusha

 

Mbunge wa Kyerwa hana ofisi

Mbunge wa Kyerwa, Mhe. Eustace Katagira, hatukuelewi, hauna ofisi, katibu wako hafahamiki, kibao kinachoonesha ofisi kimeliwa na mchwa pale Rubwera na chumba cha mbunge ni ofisi ya Mratibu Elimu Kata.

 

Tunaomba ruti ya Kivukoni-Muhimbili

Jeshi la usalama baharini tunaomba ruti ya Kivukoni-Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka Kigamboni.

Abraham, Dar es Salaam

 

 

Mwigulu Nchemba atuombe radhi

 

Mwigulu Nchemba tuombe radhi Watanzania, usipofanya hivyo utaificha wapi aibu ya kusema una ushahidi wa kutosha kuhusu ugaidi, kumbe uongo!

 

Mchangiaji wa JAMHURI, Dar

 

 

Barabara Nzega-Tabora kero tupu

 

Barabara ya Nzega-Tabora ni kero, ni mbovu kupita kiasi. Serikali inafanya nini kiasi cha kutotuondolea kero hii?

 

Kapaya Ilagila, Nzega

 

 

RC Dar es Salaam amekurupuka

 

Viashiria vya uvunjifu wa amani; kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu kanda zinazokashfu dini haioneshi dhamira chanya kwa kiongozi wa Serikali isiyo na dini anaposema, “Kama una kanda hizo sikiliza chumbani kwako.”

 

Mpenda amani, Shinyanga

 

 

Waajiri aina ya Ndygai ni wengi

 

Waajiri aina ya Mhe. Ndugai ni wengi, (majina tunayahifadhi) wanafukuza watu kinyama. Wananyanyasa sana wanyonge.

 

Mdau wa JAMHURI, Dar

1108 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!