Polisi iwakamate waliomuua Barlow

Ili Jeshi la Polisi liweze kujijengea hesima katika jamii, lioneshe makali yake katika kushughulikia mtandao wa mauaji ya RPC Liberatus Barlow, kufuatia maelezo yaliyotolewa na Malele.

Boniface Nyerere, Dar

Maofisa Maliasili ndiyo wavuvi haramu

Nimelalamika kwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuhusu uvuvi haramu ukiwamo wa kutumia sumu katika Ziwa Victoria unaofanywa na baadhi ya maofisa wa Maliasili mkoani Mwanza, lakini sijajibiwa!

Msimamizi rasilimali Ziwa Victoria

 

Msiifanye Kyerwa shamba la bibi

Chonde chonde madiwani wa Halmshauri mpya ya Kyerwa, tujiepushe na matatizo ya ukabila, ukanda, ufisadi na ubabe.

 

Msiifanye Kyerwa shamba la bibi, leteni maendeleo kwa wananchi tuko nyuma yenu, hii ni Kyerwa sio Karagwe tena.

Mpenzi wa JAMHURI, Kyerwa

 

Ninawakosoa wabunge wa CHADEMA

CHADEMA inaweka changamoto sana bungeni, lakini inakera pale baadhi ya wabunge wake wanapokosa nidhamu kupindukia. Wapunguze jazba.

Mkereketwa wa ustaarabu, Pwani

 

Mbunge Musoma Vijijini unazijua kero hizi?

Wanakijiji wa Sirori Simba wamenyang’anywa ardhi ya Kiryenyi, wamekosa pa kulima, watakufa kwa njaa. Vituo vya afya havina dawa na miundombinu ni mibovu. Je, mbunge wetu unayajua haya.

Marwa Martin, Musoma Vijijini

 

RPC Mkoa Kusini mwondoe trafiki huyu

RPC Mkoa wa Kusini tunakuomba umwondoe Mkuu wa Trafiki Wilaya ya Kati, analichafua Jeshi la Polisi kwa kuendekeza tabia ya kuomba rushwa kutoka kwa watuhumiwa wa ukiukaji sheria za usalama barabarani.

Mdau wa Jamhuri – Machui, Zanzibar

 

Polisi Loliondo uozo mtupu

Jeshi la Polisi Loliondo ni uozo mtupu, baadhi ya askari wamegeuka kuwa majambazi. Bunduki za Serikali zinatumika katika matukio ya uhalifu usiku na kurudishwa asubuhi. Tunaomba IGP Said Mwema awamulike.

Mkereketwa, Liliondo

 

Waziri wa Elimu ajiuzuru

Sakata la kufutwa kwa matokeo ya kidato cha nne 2012, Serikali ikubali kufanya kosa lililosababisha wanafunzi wengi kufeli mtahani huo, hivyo waziri mwenye dhama ajiuzulu, sio kulitupia lawama Baraza la MItihani Tanzania.

Mzazi, Lindi

 

Siungi mkono TV kwenye magari

Fuatilieni tangazo kuhusu TV kwenye magari. Hivi magari yanapohalalishiwa kuwa na TV, madereva watazingatia sheria za usalama barabarani?

Kauga, Tabora

 

1035 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!